Nov 17, 2023 03:20 UTC
  • Kan'ani: Waungaji mkono wa Israel hawana haki ya kuinasahi Iran kuhusu haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja azimio dhidi ya Iran kuhusu haki za binadamu lililopasishwa katika kamati ya tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa ni kinyume cha sheria na lilsilokubalika hata kidogo.

Nasser Kan'ani Chafi amesema hayo katika radiamali yake kwa hatua yenye utashi wa kisiasa ya baadhi ya madola ya Magharibi ya kupendekeza na kupasisha azimio dhidi ya Iran kuhusiana na haki za binadamu na kusema kuwa, nchi hizi zenye historia ndefu ya ukiukaji wa haki za binadamu hazina ustahiki na hadhi ya kutoa nasaha kwa serikali na watu wa Iran kuhusiana na  haki za binadamu.

Rasimu ya azimio lililopendekezwa la Kanada kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran limepasishwa kwa kura 80 za ndio, kura 29 za kulipinga na huku mataifa 65 yakijizuia kupiga kura katika Umoja wa Mataifa.

 

Kuhusiana na hilo, Nasser Kanani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya kisiasa ya baadhi ya nchi za Magharibi katika kuwasilisha na kuidhinisha azimio la haki za binadamu dhidi ya Iran katika Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na wakati huohuo kufumbia macho na kupuuza kabisa jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza ni fedheha kubwa.

Aidha amesema hatua hiyo inaonyesha unafiki na uwongo wao wa wazi wa madai yao kutetea haki za binadamu na kulichukulia azimio hilo kuwa halina thamani na si lenye kukubalika.

Tags