Apr 06, 2024 10:34 UTC
  • Mbali na jinai nyinginezo, Israel inawashikilia mamia ya watoto wa Palestina kwenye jela za kutisha

Klabu wa Mateka wa Palestina imesema kuwa, mbali na jinai zake nyinginezo nyingi zisizo na mfano, utawala wa Kizayuni unawashikilia mamia ya watoto wadogo wa Palestina katika jela zake za kuogofya.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo Jumamosi na kuinukuu klabu hiyo ikisema kuwa, hivi sasa watoto wadogo 2000 wanashikiliwa kwenye jela hizo za kutisha za Wazayuni mbali na utawala huo katili kuua maelfu ya watoto na wanawake kwenye kipindi cha miezi sita ya mashambulizi ya kila upande huko Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tangu Israel ilipoanzisha jinai zake mpya dhidi ya Wapalestina hasa wa Ukanda wa Ghaza tarehe 7 Oktoba 2023 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni umeshateka nyara zaidi ya watoto 500 wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan pekee.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Israel ndio utawala pekee katili duniani ambao kila mwaka unawapandisha kwenye mahakama za kijeshi baina ya watoto 500 hadi 700 wa Kipalestina na dunia inanyamazia kimya jinai hizo. 

Kabla ya hapo Klabu ya Mateka wa Palestina ilikuwa imetangaza kuwa, tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi hivi sasa wimbi la kutekwa nyara Wapalestina na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni limeongezeka kwa namna ya kutisha kiasi kwamba maelfu ya Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wameshatekwa nyara na Wazayuni tangu wakati huo hadi hivi sasa.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza jinai zake za kutisha dhidi ya Wapalestina hasa wa Ukanda wa Ghaza kutokana na uungaji mkono wa pande zote wa madola ya Magharibi hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Tags