Apr 25, 2024 02:44 UTC
  • Jeshi la Israel laendeleza mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

Jeshi la utawala ghasibu wa Israel limeua raia zaidi Wapalestina huku likiendeleza vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza

Watu watatu wameuawa baada ya ndege za kivita za Israel kushambulia jengo la makazi katika kitongoji cha al-Salam cha mji wa Rafah kusini mwa Gaza.

Ndege za Israel pia ziliua watu watano kutoka kwa familia moja iliyokuwa imekimbilia hifadhi ndani ya nyumba katika kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat katikati mwa Gaza. Kambi hiyo imekuwa ikilengwa kila siku na jeshi katili la Israel karibu kila siku katika wiki chache zilizopita.

Hayo yamejiri wakati ambao Jumatano ya jana ilikuwa siku ya 201 tangu Israel ianzishe vita vya mauaji ya kimbari Gaza Oktoba 7 .

Tokea wakati huo jeshi katili limeua shahidi Wapalestina 34,183 na wengine 77,143 pia wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo. Wizara ya Afya ya Palestina inasema wanawake na watoto ni asilimia 72 ya wahasiriwa.

Licha ya kampeni ya umwagaji damu na uharibifu, hadi sasa utawala huo umeshindwa kufikia "malengo" yake, ambayo iliyatangaza kuwa ni kuuwaachilia mateka, ambao walitekwa wakati wa Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa, kuangamiza harakati ya Kiislamu za kupignaia ukombozi wa Palestina huko Gaza, na kuwalazimisha wakazi wote wa Palestina kuhamia nchi jirani ya Misri.