Apr 25, 2024 06:06 UTC
  • Idadi ya Wazayuni wanaoomba misaada ya kisaikolojia yaongezeka

Televisheni ya utawala wa Kizayuni imetangaza ongezeko la mara nne la maombi ya yanayotolewa na Wazayuni kwa ajili ya kupata misaada ya kisaikolojia kufuatia operesheni ya Iran ya Ahadi ya Kweli ya kuuadhibu utawala huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, baada ya operesheni ya adhabu ya Ahadi ya Kweli katika kujibu shambulio la utawala haramu wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus, Syria idadi ya Wazayuni wanaoomba msaada wa kiakili na kisaikolojia imeongezeka mara nne.

Hapo mwanzo, gazeti la Yediot Aharonot lilitoa ripoti  kuhusu wasiwasi wa kuporomoka kwa mfumo wa afya ya akili wa utawala haramu wa Kizayuni.

Gazeti hilo la Kizayuni limeandika kuwa: 'Sambamba na kuongezeka maombi ya huduma za magonjwa ya akili katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel), utawala haramu huu unakabiliwa na uhaba wa madaktari wa magonjwa ya akili na madaktari mahiri katika uwanja huo.'

 

Kabla ya hapo, chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kilitoa ripoti juu ya mgogoro usio na kifani wa matatizo ya akili katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na wito wa Wizara ya Afya ya utawala wa Kizayuni wa kutaka kumvutia mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa hofu na woga.

Katika sehemu nyingine ya ripoti hiyo  imeelezwa kuwa, zikiwa zimepita siku 200 tangu kushindwa jeshi la Kizayuni kufikia malengo yake katika vita huko Ghaza, Wazayuni wamekuwa wakitoa wito wa kufanyika maandamano mjini Tel Aviv serikali  ya Netanyanhu.

Kuhusiana na suala hilo, msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, Abu Obeidah, alisisitiza  Jumanne akisema, utawala huo  wa Kizayuni licha ya kupita siku 200 tangu kuanza kwa vita hivyo, na bila kufikia malengo yoyote, umekwama kwenye kinamasi cha ukanda wa Gaza, na unaendelea tu na mauaji na uharibifu zaidi katika maeneo hayo.

Vyombo vya habari vya huko Palestina vilitangaza hapo awali kwamba: kwa kufukuliwa idadi nyingine ya miili ya mashahidi wa Kipalestina kutoka kwenye makaburi ya halaiki katika eneo la Hospitali ya Nasser huko Khan Younis, idadi ya miili iliyofukuliwa imefikia 310.

Vyombo hivyo vya habari hivi vimewanukuu maafisa wa Palestina wakisema kuwa; huenda mamia zaidi ya miili ya watu waliotoweka ikafukuliwa kwenye makaburi hayo.

Kabla ya hapo  Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina pia ilitangaza kuwa kufuatia kuondoka jeshi la utwala wa  Kizayuni katuika baadhi ya maeneo ya Gaza, idadi ya miili iliyopatikana katika kaburi la umati iliyogunduliwa Jumamosi iliyopita, katika eneo la Nasser Medical Complex katika mji wa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, imeongezeka hadi kufikia 283.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Stephen Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) amesema ripoti zilizotolewa za kugunduliwa kwa kaburi la umati katika Ukanda wa Gaza zinatia wasiwasi.