May 09, 2019 04:27 UTC
  • Maradhi ya kisaikolojia yaongezeka kati ya Wazayuni kutokana na ngoma ya vita ya Netanyahu

Kanali ya 12 ya utawala Kizayuni wa Israel imekiri kwamba kutokana na vita vya hivi karibuni, maradhi ya kisaikolojia na kiroho yameongezeka kati ya walowezi wa Kizayuni na kwamba sasa wanatibiwa kwa njia ya mazungumzo ya video.

Kanali hiyo imemnukuu Eli Beer, kiongozi wa taasisi ya Kizayuni inayoitwa 'Umoja wa Wokovu' akisisitiza kwamba, hali ya mambo upande wa kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ni mbaya sana na hivyo imeisababishia mzigo mzito serikali ya Tel Aviv. Beer amebainisha kwamba kwa sasa kunahitajika vituo vingi vya matibabu kwa ajili ya kuwasaidia walowezi wa Kiyahudi ambao kutokana na vita vya hivi karibuni wamepatwa na matatizo ya kisaikolojia. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kizayuni tayari nchi kadhaa zimetangaza utayarifu wao kwa ajili ya kutoa msaada wao kwa walowezi hao kupitia njia ya video.

Utawala wa Kizayuni uliojengeka katika misingi ya ugaidi na ukandamizaji

Ripoti hiyo imeeleza kwamba wakazi wa vitongoji vya karibu na Ukanda wa Gaza, ndio walioathirika zaidi kutokana na vita vya hivi karibuni kati ya Israel na wanamuqawama wa Kipalestina na kwamba aghalabu wameathirika kiroho. Matatizo ya kiroho na kisaikolojia kati ya askari wa Kizayuni nayo pia yameshika kasi, suala lililopelekea kuongezeka kiwango cha askari wanaojiua kati yao. Aidha vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza kwamba mwaka 2018 jumla ya askari tisa walijiua, huku wengine 16 wakiwa walijiua mwaka 2017 wakiwemo makanda jeshini.

Tags