Dec 26, 2020 02:45 UTC
  • Nouri al-Maliki: Qassem Suleimani alifelisha njama za kubadilisha utambulisho wa eneo

Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq Nouri Al-Maliki amesema, kwa mapambano, uvumlivu mkubwa na jihadi yake, shahid Qassem Suleimani aliweza kufelisha na kuzima njama nyingi za maadui za kutaka kubadilisha utambulisho wa eneo la Asia Magharibi.

Kanali ya televisheni ya Al-Alam imeripoti kuwa, Nouri Al-Maliki ameyasema hayo sambamba na kukaribia hauli na maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu alipouawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na akabainisha kwamba, shahid Suleimani aliyasaidia mataifa na harakati zingine za mapambano ili ziweze kusimama imara kwa umoja na kwa muqawama kukabiliana na mipango na njama za maadui.

Nouri Al-Maliki

Al Maliki amesema, shambulio la mauaji ya kigaidi ya shahid Qassem Suleimani ilikuwa jinai chafu iliyofanywa na nchi ambayo hujinasibu kila mara kuwa ni mtetezi wa uhuru na demokrasia na akasisitiza kwamba, serikali ya Iraq inapaswa kufuatilia faili la mauaji hayo kwa uzito mkubwa.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020 alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa shahidi katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini humo.../

Tags