Jul 06, 2021 08:16 UTC
  • Ubalozi wa Marekani Baghdad washambuliwa kwa droni

Baadhi ya duru za habari za Iraq zimetangaza habari ya kujiri shambulio la anga katika eneo la Kijani huko Baghdad na karibu na jengo la ubalozi wa Marekani.

Tovuti ya habari ya Saberin News imeandika kuwa: kengele za tahadhari zimesikika katika kituo cha tatu cha al Tawhid katika ubalozi wa Marekani katika Ukanda wa Kijani mjini humo. Duru hizo za habari zimeongeza kuwa, shambulio kali limetekelezwa katika kituo cha tatu al Tawhid katika ubalozi wa Marekani na kwamba ngao ya ulinzi ya 30- RAM  imejaribu kukilinda kituo hicho na shambulio jingine jipya.   

Hii ni katika hali ambayo jana alasiri pia kituo cha anga cha jeshi cha Ain al Asad katika mkoa wa an Anbar Iraq kilishambuliwa kwa maroketi nane. 

Tovuti ya habari ya Saberin awali ilikuwa imeripoti kuwa, milipuko kadhaa imetokea katika kambi ya wanajeshi vamizi wa Marekani katika karakana moja ya kuzalisha gesi huko Deir-Zor. Mashambulizi dhidi ya misafara ya wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq yangali yanaendelea huku Washington ikifanya kila iwezalo kuakhirisha mazungumzo ya kistratejia kati yake na Iraq kwa ajili ya kuondoa wanajeshi wake huko Iraq. 

Wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq 

Wananchi na makundi mengi ya Iraq wanataka kuondoka wanajeshi magaidi wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Bunge la Iraq pia tayari limepasisha mpango wa kuondoka wanajeshi hao nchini humo. 

Tags