Jun 01, 2023 06:14 UTC
  • Wapalestina 45 wajeruhiwa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi

Taasisi ya Mwezi Mwekundu ya Palestina jana usiku ilitangaza kuwa Wapalestina 45 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya wanajeshi wa Kizayuni na raia wa Palestina katika mji wa Nablus kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kila siku huwaua shahidi, kuwajeruhi au kuwatia mbaroni wananchi madhlumu wa Palestina kwa visingizio mbalimbali; ambapo Wapalestina pia hutekeleza oparesheni dhidi ya Wazayuni katika kujibu jinai hizo. 

Shirika rasmi la habari la Iran, IRNA limearifu kuwa, walowezi wa Kizayuni huku wakisadiwa na wanajeshi wa Israel wamepigana na Wapalestina katika eneo la Burqa na katika vijiji vya kandokando huko kaskazini magharibi mwa mji wa Nablus' ambapo Taasisi ya Mwezi Mwekundu ya Palestina imetangaza kuwa Wapalestina 45 wamejeruhiwa katika mapigano hayo.  

Juzi Jumanne pia Wapalestina 46 walijeruhiwa baada ya wanajeshi ghasibu wa Israel kuvamia kambi ya zamani ya Askar mashariki mwa Nablus na katika kambi ya Nur Shams huko mashariki mwa Tul-Karm kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan inayokaliwa kwa mabavu.  

Shambulio la Wazayuni katika kambi ya Nur Shams 

Huko nyuma Wazayuni walikuwa wakipigana na Wapalestina katika maeneo ya kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na katika Ukanda wa Ghaza tu, lakini  hivi sasa eneo la Ukingo wa Magharibi huko mashariki mwa Palestina limekuwa maficho ya Wazayuni waoga kutokana vijana wa eneo hilo kujizatiti kwa silaha.