-
Pretoria: Tunatiwa wasi wasi na mauaji ya kigaidi ya Israel
Sep 29, 2024 10:45Afrika Kusini imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja nchini Lebanon, ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza mashambulio ya anga hivi karibuni, na kuua mamia ya raia huku maelfu ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.
-
Papa awataka Wakatoliki Marekani wachague 'uovu ulio afadhali kidogo' kati ya Trump na Harris
Sep 13, 2024 23:58Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewahimiza Wakatoliki nchini Marekani wakapige kura katika uchaguzi wa Novemba, akisema wanapaswa "kuchagua uovu ulio afadhali kidogo" huku akiwakosoa wagombea wote wawili wakuu wa kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo.
-
Wafanyakazi 6 wa UN miongoni mwa watu 18 waliouliwa katika shambulio la kinyama la Israel Ghaza
Sep 12, 2024 04:10Wafanyakazi sita wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) ni miongoni mwa watu 18 waliouawa hapo jana katika shambulizi la kinyama lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika skuli inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Ghaza ya Kati.
-
Ofisi ya Rais Afrika Kusini: Tutafuatilia mashtaka yetu dhidi ya mauaji ya kimbari ya Israel
Sep 11, 2024 22:59Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imetangaza katika taarifa yake kwamba, itaendelea kufuatilia kesi ya mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) hadi hukumu yake itakapotolewa.
-
Wakulima wa Afrika Kusini watuhumiwa kuuwa wanawake 2, na kisha miili yao kuwalisha nguruwe
Sep 10, 2024 23:42Wanaume watatu nchini Afrika Kusini wanatuhumiwa kuwauwa wanawake wawili na kisha miili yao kuwalisha nguruwe katika shamba lao. Kesi hii tajwa imeibua ghadhabu na hasira miongoni mwa jamii ya Afrika Kusini.
-
Wafuasi wa chama cha Jacob Zuma wapoteza maisha katika ajali
Aug 31, 2024 23:25Wafuasi sita wa chama cha upinzani cha MK kinachoongozwa na Jacob Zuma nchini Afrika Kusini, wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea siku ya Jumamosi, mashariki mwa nchi hiyo.
-
Wanaharakati waitaka Afrika Kusini iiwekee Israel vikwazo vya biashara
Aug 25, 2024 22:59Wanaharakati wameitaka Afrika Kusini iuwekee utawala wa Kizayuni wa Israel vikwazo vya kibiashara na kusimamisha mara moja mauzo ya nje ya bidhaa zake kwa utawala huo pandikizi.
-
Takriban wahamiaji 100 wa Ethiopia waokolewa na polisi nchini Afrika Kusini
Aug 05, 2024 10:15Polisi ya Afrika Kusini imeeleza kuwa imewaokoa wahamiaji 90 wa Kiethiopia waliokuwa wakishiliwa kwenye nyumba moja kinyume na ridhaa yao katika mji wa Johannesburg.
-
Afrika Kusini yailaani Israel kwa kumuua kigaidi Ismail Haniyah
Aug 01, 2024 23:14Serikali ya Afrika Kusini imelaani vikali mauaji ya kigaidi ya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniyah.
-
Mandela: Houthi wazidishe mashambulizi ili kuikomboa Palestina
Jul 22, 2024 07:28Mjukuu wa Nelson Mandela, shujaa na kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ametoa mwito kwa Harakati ya Ansarullah na vikosi vya wanajeshi wa Yemen kushadidisha operesheni zao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuua watoto na wanawake wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.