-
Mtoto wa miezi 8 ni mmoja wa Wapalestina waliouawa na jeshi katili la Israel
May 16, 2018 03:21Mtoto mwenye umri wa miezi minane tu ni mmoja wa wahanga wa ukatili wa hivi punde wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Arab League yaitisha kikao cha dharura kujadili mauaji ya umati ya Wapalestina
May 16, 2018 03:00Huku nchi mbalimbali za dunia zikiendelea kulaani vikali mauaji ya umati yaliyofanywa na askari wa utawala bandia wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeaitisha kikao cha dharura kujadili ukatili huo.
-
Wito wa Hamas katika kukaribia mwaka wa 70 wa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina
May 13, 2018 22:37Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa taarifa katika kukaribia maadhimisho ya kutimia mwaka wa 70 tangu kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina yaani tarehe 15 Mei na kuwatolea mwito wananchi wa Palestina kushiriki kwa wingi katika maandamano ya "Haki ya Kurejea" huko Quds, katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan, Ukanda wa Ghaza na ardhi za Palestina zilizoanza kukaliwa kwa mabavu mwaka 1948.
-
Baraza la Usalama latakiwa kuichukulia hatua Israel kwa kuwaua Wapalestina
Apr 28, 2018 03:07Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo liuchukulie hatua mara moja utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kuwaua shahidi Wapalestina wanaofanya maandamano ya amani katika mpaka wa Ghaza.
-
Mkuu wa Haki za Binadamu UN alaani ukatili wa Israel huko Ghaza
Apr 27, 2018 09:22Mkuu wa masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa ameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutumia nguvu ziada dhidi ya waandamanaji Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza jambo ambalo limepelekea makumi kuuawa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
-
Balozi wa Palestina UN ataka kuchunguzwa jinai za Israel huko Gaza
Apr 20, 2018 23:40Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa umoja huo kuunda kamisheni huru ya kuchunguza jinai za kutisha zinazofanywa na wanajeshi katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Hamas: Kutunguliwa ndege za Israel Gaza, ni ishara ya kuwa macho muqawama
Apr 12, 2018 10:04Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kitendo cha harakati hiyo kufanikiwa kutungua ndege za kijeshi za utawala wa Kizayuni wa Israel zinazoshambulia Ukanda wa Gaza ni ithibati tosha kuwa harakati hiyo ya muqawama imesimama kidete na iko tayari kuzima chokochoko na uvamizi wa Tel Aviv.
-
Mtazamo wa Hassan Nasrullah kuhusiana na uchaguzi wa bunge nchini Lebanon
Apr 11, 2018 02:52Jumapili iliyopita Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon alihutubia eneo la Nabatieh kusini mwa Lebanon ambapo alibainisha maoni yake kuhusiana na uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.
-
Ukosoaji mkali wa kiongozi wa chama cha Leba cha Uingereza kwa hatua za kinyama za Israel dhidi ya Wapalestina
Apr 09, 2018 01:27Jeremy Corbyn, kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza amelaani mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa maandamano kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa mwenendo wa kuvifumbia macho na kuvinyamazia vitendo vya Israel vya kuwaua Wapalestina wanaoandamana bila ya kubeba silaha yoyote, inapasa ukomeshwe.
-
Arab League nayo yataka Israel ipelekwe The Hague
Apr 04, 2018 21:08Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (The Arab League (AL) nayo imejiunga na harakati na taasisi nyingine za kikanda na kimataifa zilizolaani jinai dhidi ya binadamu zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na imeutaka Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi la Isrel dhidi ya raia wa Palestina.