-
Iran yalaani mashambulio ya silaha nchini Niger
Mar 20, 2021 04:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mashambulio yaliyofanywa hivi karibuni na wabeba silaha nchini Niger, ambayo yamepelekea makumi ya watu kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.
-
Iran: Hatujapokea ujumbe wowote kutoka Marekani
Mar 20, 2021 04:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haijapokea ujumbe wowote kutoka kwa Marekani wala haina azma yoyote ya kuitumia Washington ujumbe.
-
Guterres alaani chuki dhidi ya Waislamu, anukulu aya ya Qur’ani
Mar 20, 2021 04:29Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu (Islamophobia) na kusema ubaguzi wa rangi kwa bahati mbaya sana upo na unaendelea katika nchi zote na katika jamii zote duniani na mizizi yake imekita kutokana na karne na karne za ukoloni na utumwa.
-
Kuendelea siasa za uhasama za Marekani dhid ya Iran
Mar 20, 2021 04:24Ikiwa ni katika kuendeleza siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wizara ya Fedha ya Marekani imewatuhumu raia wengine 10 wa Iran kuwa wamekiuka vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran.
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais Magufuli
Mar 20, 2021 01:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za mkono wa pole kwa wananchi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
-
Qalibaf: Ni lazima Marekani iondoe vikwazo vyote dhidi ya Iran
Mar 19, 2021 08:48Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: "Marekani inapaswa kuondoa vikwazo vyote ili Iran iweze kutekeleza ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA."
-
Iran yaadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam Hussein (AS)
Mar 17, 2021 04:03Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeungana na ulimwengu wa Kiislamu hii leo kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume wetu mtukufu Muhammad (SAW).
-
Iran yakosoa undumakuwili wa Uingereza, yataka silaha zote za nyuklia ziharibiwe
Mar 17, 2021 03:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali undumakuwili wa Uingereza; ambayo kwa upande mmoja inatoa madai yasiyo na msingi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani na kwa upande mwingine, inasema kuwa inataka kuongeza akiba ya silaha zake za nyuklia.
-
IAEA yataka washiriki wa JCPOA wakumbatie fursa waliyopewa na Iran
Mar 17, 2021 03:03Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran ni 'magumu lakini yanatekelezeka' huku akizitaka pande husika za JCPOA kukumbatia muhula wa miezi mitatu ziliopewa na Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya kuyanusuru mapatano hayo.
-
Iran yakanusha kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani
Mar 17, 2021 01:00Duru za kiusalama nchini Iran zimekadhibisha madai ya Marekani kwamba kuna mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yanayoendelea baina ya Tehran na Washington.