Kuendelea siasa za uhasama za Marekani dhid ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i68094-kuendelea_siasa_za_uhasama_za_marekani_dhid_ya_iran
Ikiwa ni katika kuendeleza siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wizara ya Fedha ya Marekani imewatuhumu raia wengine 10 wa Iran kuwa wamekiuka vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 20, 2021 04:24 UTC
  • Kuendelea siasa za uhasama za Marekani dhid ya Iran

Ikiwa ni katika kuendeleza siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wizara ya Fedha ya Marekani imewatuhumu raia wengine 10 wa Iran kuwa wamekiuka vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran.

Wizara hiyo imetangaza kwamba raia hao 10 wa Iran wamekiuka vikwazo hivyo kwa kufanya miamala ya siri yenye thamani ya dola milioni 3000 kwa manufaa ya Iran na pia kubuni mashirika bandia nchini Canada, Hong Kong na Imarati kwa ajili ya kukwepa vikwazo vya Marekani vilivyowekwa dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, iwapo raia hao watathibitika mahakamani kuwa walihusika na miamala hiyo watatambuliwa kuwa ni wahalifu na hivyo kupewa adhabu kali ya kifungo cha jela cha miaka 20.

Wizara ya Fedha ya Marekani

Katika kudumisha sias zake za uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, serikali ya Marekani imeiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vikali vya kiuchumi kwa lengo la kuifanya asalimu amri mbele ya matakwa yake haramu. Mahakama za Marekani zimekuwa zikitoa hukumu na kuwapa adhamu kali raia wa Iran kwa visingizio mbali mbali visivyo na msingi wowote wa kieshria.