-
Qalibaf: Iran haitasubiri barua yoyote kutoka Marekani
Mar 09, 2025 07:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Jamhuri ya Kiislamu haisubiri barua yoyote kutoka kwa Marekani, kwani taifa hili linategemea uwezo wa ndani katika kukabiliana na changamoto zake.
-
Iran: Machafuko nchini Syria ni kwa manufaa ya Israel
Mar 09, 2025 03:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, machafuko na ukosefu wa utulivu nchini Syria ni kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni na kwamba magenge ya kigaidi na yenye misimamo mikali yanatumia vibaya fursa hiyo kwa manufaa yao binafsi.
-
Siku ya Wanawake; Iran yataka Israel itimuliwe UN + Picha
Mar 09, 2025 03:16Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetaka utawala wa Kizayuni utimuliwe kutoka kwenye umoja huo kutokana na jinai kubwa unazofanya dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Araghchi: Kuundwa nchi moja ya kidemokrasia ndiyo suluhu ya kadhia ya Palestina
Mar 08, 2025 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza tena msimamo wa Tehran wa kupinga eti 'suluhisho la mataifa mawili' kuwa njia ya kupata haki za Wapalestina na kusisitiza kwamba, uungaji mkono usioyumba wa Iran kwa kadhia ya Palestina bado upo thabiti.
-
Russia: Israel haina haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Iran
Mar 08, 2025 00:54Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa mjini Vienna, Mikhail Ulyanov, amesema kuwa utawala wa Israel hauna haki ya kutoa maoni kuhusiana na mpango wa amani wa nyuklia wa Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha
Mar 07, 2025 07:43Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, kufanya mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha. Amesisitiza kuwa, taifa la Iran ni la hamasa ya Karbala na 'Ashura na kamwe halikubali kudhalilishwa.
-
Iran yateuliwa Makamu wa Rais wa OPCW licha ya upinzani wa Marekani
Mar 07, 2025 07:16Iran imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Utendaji la Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) licha ya Marekani kufanya juu chini kuzuia Jamhuri ya Kiislamu kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.
-
Iran: Kufurushwa Wapalestina Gaza ni muendelezo wa mauaji ya kimbari
Mar 06, 2025 23:03Iran imesema kuwa, mpango wa kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Gaza na kuwapeleka katika nchi jirani ni kuendeleza mauaji ya kimbari kwa kutumia zana za kisiasa.
-
Mjumbe wa Iran IAEA: Kampeni ya mashinikizo ya Magharibi dhidi ya Iran haina tija
Mar 06, 2025 02:17Balozi na Mwakilishi wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameonya kuwa, mkakati wa Magharibi wa kutoa mashinikizo kwa Tehran na kuilazimisha kutekeleza kwa upande mmoja majukumu ya kinyuklia "sio tu kwamba haufanyi kazi bali pia hauna tija" .
-
Russia yaitaka Ulaya iache vitisho dhidi ya Iran
Mar 05, 2025 22:59Russia imekosoa vikali vitisho vya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani vya kuamilisha mchakato wa kurejesha vikwazo dhidi ya Iran na kutaja msimamo huo kuwa wa "kutowajibika" na "ulio kinyume cha sheria".