-
Iran: Tutajibu iwapo Israel itarusha hata mshale jangwani
Oct 30, 2024 23:07Vyombo vya ulinzi vya Iran vimesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itajibu mapigo ya uchokozi wowote wa Israel dhidi ya ardhi yake, hata kama hatua hiyo ni ndogo na isiyo na tija, kama kurusha mshale kuelekea kwenye jangwa moja la nchi hii.
-
Iran: Tunao uwezo wa kuishambulia Israel kwa 'darzeni' za operesheni sawa na "Ahadi ya Kweli"
Oct 30, 2024 10:04Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema Iran inao uwezo wa kuteketeza 'darzeni' za operesheni za kulipiza kisasi sawa na "Operesheni ya Ahadi ya Kweli" iliyotekeleza mwezi Aprili kulenga maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Palestina unayoikalia kwa mabavu.
-
Malalamiko ya wajumbe wa Baraza la Usalama dhidi ya ushirikiano wa Marekani na utawala wa Kizayuni
Oct 30, 2024 06:35Katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika karibuni kwa ajili ya kijadili suala la hujuma ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, nchi nyingi zikiwemo Algeria, China, Russia, Iraq na Syria zimelaani vikali kitendo hicho cha uchokozi na kutaka uchokozi huo ukomeshwe mara moja.
-
Iran: Tuna haki halali ya kujilinda na kujihami
Oct 30, 2024 00:00Msemaji wa serikali ya Iran, Fatemeh Mohajerani amesema Jamhuri ya Kiislamu ina haki ya kujilinda na kusisitiza kuwa, nchi hii itatekeleza haki hiyo "halali" kwa "wakati na mahali mwafaka."
-
Araghchi: Baraza la Usalama linapasa kuiwekea vikwazo Israel
Oct 30, 2024 00:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina jukumu la kuuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na tabia ya utawala huo kuendelea kushupalia vita na umwagaji damu huko Gaza na Lebanon.
-
Rais Pezeshkian: Iran itatoa jibu linalostahiki kwa uchokozi wa Israel dhidi yake
Oct 28, 2024 03:25Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haipendi vita lakini iko imara katika kujihami na kulinda usalama wa wananchi wake na itatoa jibu linalostahiki kwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni dhidi yake.
-
Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama kuhusu shambulio la kigaidi kusini mashariki mwa nchi
Oct 27, 2024 23:28Balozi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja huo na kulitaka litoe azimio la kulaani shambulio la kigaidi la genge linalojiita "Jeysh al Adl" katika mkoa wa Sistan na Baluchistan wa kusini mashariki mwa Iran.
-
Rais Pezeshkian: Wairani watajibu chokochoko za maadui dhidi ya nchi yao
Oct 26, 2024 23:40Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ametoa rambirambi zake kufuatia kuuawa shahidi maafisa usalama wa nchi hii katika mashambulizi ya kichokozi ya jana Jumamosi ya utawala wa Kizayuni na kundi la kigaidi linaloungwa mkono na maajinabi.
-
Tehran: Tuna haki halali ya kujihami mkabala wa uvamizi wa Wazayuni
Oct 26, 2024 07:22Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali hatua ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni ya kushambulia baadhi ya vituo vya kijeshi hapa nchini, na kuitaja kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
-
Iran yasema iko tayari kujibu uchokozi na uvamizi wa Israel
Oct 26, 2024 06:32Duru za kuaminiki zimeliambia shirika la habari la Tasnim kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ipo tayari na imejiandaa kujibu chokochoko za utawala wa Kizayuni wa Israel.