-
Uchunguzi: Marekani ilishinikiza kutimuliwa kamanda wa Kenya, Sudan Kusini
Nov 20, 2016 04:40Uchunguzi uliofanywa na shirika moja la kimataifa la kutathmini masuala ya sera umefichua kuwa, Marekani ilishinikiza kufutwa kazi kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Kenya aliyekuwa akisimamia Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS).
-
Kuafiki Kenya uakhirishaji tarehe ya kufunga kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Dadaab
Nov 18, 2016 04:39Hatimaye baada ya mazungumzo magumu, serikali ya Kenya wiki hii imeafiki kuakhirisha tarehe ya kufungwa kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Somalia.
-
Kenya yaakhirisha tarehe ya kufunga kambi ya Dadaab
Nov 16, 2016 10:16Kenya imerefusha muda wa kuwarejesha makwao wakimbizi wa Somalia walioko katika kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa nchi, ambayo ilitazamiwa kufungwa kikamilifu kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
-
Amnesty yaikosoa Kenya kwa kuwafukuza wakimbizi kutoka Somalia
Nov 15, 2016 10:45Shirika la haki za binadmau la Amnesty International limeikosoa serikali ya Kenya kwa kuwalazimisha wakimbizi kutoka Somalia kurejea katika nchi yao inayokumbwa na vita na hivyo kuhatarisha maisha yao.
-
Kuondoka askari wa kulinda amani wa Kenya huko Sudan Kusini
Nov 10, 2016 09:39Katika hali ambayo, vita na mapigano yanaendelea kushuhudiwa katika nchi ya Sudan Kusini, suala la kuondoka nchini humo baadhi ya askari wa kusimamani amani limegeuka na kuwa changamoto nyingine inayoikabili nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
Machar aikosoa Kenya kwa kumtimua msemaji wake
Nov 05, 2016 00:06Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini ameijia juu serikali ya Kenya kwa kumtimua nchini humo msemaji wake James Gatdet Dak na kusisitiza kuwa hatua hiyo imekiuka Hati ya makubaliano ya Geneva.
-
Uhuru: Kenya haijutii kuwaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini
Nov 03, 2016 12:57Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema taifa hilo halijuti kwa uamuzi wake wa kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki walioko Sudan Kusini chini ya mwavuli wa kikosi maalumu cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa (UNMISS).
-
Tanzania na Kenya zakubaliana kujenga barabara mbili unganishi
Nov 01, 2016 04:27Tanzania na Kenya zimekubaliana kuanza kwa wakati ujenzi wa barabara mbili unganishi ambazo zitaboresha usafirishaji wa bidhaa na safari za raia kati ya nchi mbili hizo.
-
Jeshi la Kenya laua magaidi 140 wa Al Shabab nchini Somalia
Oct 31, 2016 23:13Jeshi la Ulinzi la Kenya, KDF, limetangaza kuwaua magaidi 140 wa kundi la kitakfiri la Al Shabab katika jimbo la Lower Jubba, mjini Afamadow nchini Somalia.
-
Rais Magufuli: Kenya, mshirika nambari moja wa Tanzania kibiashara barani Afrika
Oct 31, 2016 11:43Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amekanusha madai kuwa serikali yake inazipuuza nchi jirani na kujikita zaidi katika masuala ya ndani.