-
Indhari ya Russia kuhusu kufutwa makubaliano ya JCPOA na taathira zake mbaya
May 05, 2018 07:39Serikali ya Russia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni utaratibu ulio na mlingano weenye manufaa ya pande zote na kutahadharisha kuwa kuvunjwa makubaliano hayo kutakuwa kwa madhara. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Russia, kuvurugwa mlingano unaolegalega wa kimaslahi ndani ya makubaliano ya JCPOA kutakuwa na taathira kuu kwa usalama wa kimataifa na muundo unaopiga marufuku uenezaji wa silaha za nyuklia.
-
Marekani yazidi kuwazatiti kwa silaha waasi nchini Syria
May 05, 2018 03:22Kwa mara nyingine tena, jana Ijumaa Marekani ilimimina shehena za silaha katika mkoa wa al Hasaka, kaskazini mwa Syria kama njia ya kuchochea vita na kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye eneo hilo.
-
Russia: Iwapo Marekani itajitoa katika JCPOA, itabidi iwekewe vikwazo
May 05, 2018 03:22Afisa mmoja wa Russia amesisitiza kuwa, kama Marekani itajitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, itabidi iwekewe vikwazo vya kimataifa.
-
Ujumbe Muhimu wa Zarif kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran + VIDEO
May 04, 2018 12:03Katika Ujumbe wake wa video hapo jana Alkhamisi, Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa kuna chaguo moja tu la kufanikisha makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita kubwa za dunia, nalo ni Marekani kutekeleza ahadi zake zote kuhusiana na makubaliano hayo.
-
Katibu Mkuu wa UN: JCPOA ni ushindi muhimu wa kidiplomasia
May 04, 2018 02:55Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya dhidi ya kuvunjwa makubaliano ya nyuklia ya Iran huku akisisitiza kuwa mapatano hayo ni ushindi muhimu wa kidiplomasia ambayo yanapaswa kulindwa.
-
Zarif: Iran haitofanya mazungumzo yoyote kuhusu JCPOA na mapatano hayo hayataongezwa chochote
May 03, 2018 23:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe alioutoa jana kwa njia ya video kwamba Tehran haitofanya mazungumzo yoyote mapya kuhusu JCPOA na wala mapatano hayo ya nyuklia hayataongezwa chochote. Amesema mapatano hayo yana njia moja tu nayo ni Marekani kuheshimu vipengee vyake vyote.
-
Muungano wa Marekani wafanya maauaji mengine ya umati nchini Syria
May 03, 2018 23:40Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani ambao unadai kupambana na magaidi wa Daeshi (ISIS) nchini Syria umefanya mauaji mengine ya umati dhidi ya raia wa mashariki mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Ripoti: Marekani imekuwa ikipigana bega kwa bega na Saudia nchini Yemen
May 03, 2018 23:25Gazeti moja la nchini Marekani limefichua kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo wamekuwa wakishirikiana moja kwa moja na Saudi Arabia katika vita nchini Yemen
-
Mwanahistoria mashuhuri wa Kiyahudi: Marekani imewafanyia hadaa watu wa Palestina
May 03, 2018 10:39Mwanahistoria mtajika wa Kiyahudi Ilan Pappé ameashiria jinsi baadhi ya Wapalestina walivyodhani kwamba Marekani ikiwa kama mpatanishi itasaidia mpango wa kuundwa nchi ya Palestina na kubainisha kuwa serikali za Marekani ikiwemo ya Barack Obama zimewafanyia hadaa watu wa Palestina.
-
Akthari ya Wamarekani: Mambo katika Ikulu ya White House yanaendeshwa shaghalabaghala
May 03, 2018 10:11Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani yanaonyesha kuwa raia wengi wa nchi hiyo wanahisi hali katika Ikulu ya White House inakwenda shaghalabaghala.