Marekani yazidi kuwazatiti kwa silaha waasi nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44070-marekani_yazidi_kuwazatiti_kwa_silaha_waasi_nchini_syria
Kwa mara nyingine tena, jana Ijumaa Marekani ilimimina shehena za silaha katika mkoa wa al Hasaka, kaskazini mwa Syria kama njia ya kuchochea vita na kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 05, 2018 03:22 UTC
  • Marekani yazidi kuwazatiti kwa silaha waasi nchini Syria

Kwa mara nyingine tena, jana Ijumaa Marekani ilimimina shehena za silaha katika mkoa wa al Hasaka, kaskazini mwa Syria kama njia ya kuchochea vita na kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye eneo hilo.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Marekani imewapelekea Wakurdi wa Syria malori mengine 10 yaliyojaa silaha katika kituo cha mafunzo ya kijeshi cha waasi hao cha Tell Beydar, kaskazini mwa nchi hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kuwapelekea shehena za silaha waasi hao wa Kikurdi wa YPG huko kaskazini mwa Syria.

Magaidi wanaofanya jinai na mauaji ya kutisha nchini Syria kwa kusaidiwa na Mrekani na vibaraka wake kama Saudi Arabia

 

Siku 20 zilizopita, Marekani iliwafikishia silaha nzito na nyepesi waasi wa Kikurdi katika eneo la Manbij, silaha ambazo sehemu yake kubwa zilitolewa zawadi na Saudi Arabia kwa waasi hao.

Muungano unaodai kuendesha vita dhidi ya ugaidi unaoongozwa na Marekani na ambao umekuwa ukifanya mashambulizi ya kiholela ndani ya ardhi ya Syria, tena bila ya ruhusa ya serikali ya nchi hiyo wala ya Umoja wa Mataifa, hivi sasa unafanya njama za kuunda kikosi maalumu cha Wakurdi kwa lengo la kulinda mipaka ya eneo linalodhibitiwa na waasi hao. Kikosi hicho kitakuwa na wanamgambo 30 elfu.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa, hadi hivi sasa Marekani imeshawapelekea magaidi wa Syria na Iraq shehena nyingi za silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola.