-
Iran: Kuipatia Israel dola bilioni 14 ni sawa na Marekani kutoa bakhshishi kwa mauaji ya Wapalestina
Feb 19, 2024 07:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuidhinishwa na Baraza la Seneti la Marekani msaada wa dola bilioni 14 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kunaonyesha kuwa Washington inautuza na kuupa bakhshishi utawala huo kwa kuwaua kwa halaiki raia wasio na hatia wa Palestina katika vita visivyo na mlingano vya Gaza.
-
Yemen: Tumeitwanga meli ya Uingereza na kuitungua ndege isiyo na rubani ya Marekani
Feb 19, 2024 07:36Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ametangaza kuwa, katika kuonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa taifa la Palestina na kujibu mashambulio na uchokozi wa Marekani na Uingereza dhidi ya ardhi ya Yemen, vikosi vya nchi hiyo vimeipiga makombora kadhaa meli ya Uingereza katika operesheni maalumu viliyotekeleza katika Ghuba ya Aden.
-
US kuipigia veto rasimu ya azimio la Algeria la kusitisha vita Gaza
Feb 18, 2024 07:35Maafisa wa Marekani wameapa kuwa nchi hiyo itatumia kura yake ya turufu kupinga rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Algeria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, la kutaka kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Biden aambiwa: Sitisha vita Gaza iwapo unataka kura za Waislamu
Feb 18, 2024 07:35Meya wa jiji la Dearborn, kaunti ya Wayne katika jimbo la Michigan nchini Marekani amesema Rais Joe Biden wa hiyo hatapata kura za Waislamu katika uchaguzi ujao nchini humo, iwapo ataendelea kuunga mkono jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza.
-
Marekani kuitumia Israel mamia ya mabomu aina ya MK-82
Feb 17, 2024 08:04Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani inapanga kutuma shehena za mabomu na silaha nyingine zenye thamani ya makumi ya mamilioni ya dola kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kumwaga damu za Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
-
Seneta wa Marekani: Washington ni mshirika wa Israel katika vita vya Gaza
Feb 14, 2024 08:48Seneta wa kujitegemea wa jimbo la Vermont nchini Marekani amesema kuwa, Washington ni mshirika wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kutokana na kuendelea kufadhili vita hivyo.
-
Kuongezeka ukosoaji wa Magharibi dhidi ya himaya ya Marekani kwa Israel katika vita vya Gaza
Feb 13, 2024 23:06Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, Jumatatu iliyopita aliitaka Marekani kuacha kutoa silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na kiwango kikubwa cha mauaji ya raia katika vita vya Gaza.
-
Venezuela yaalani kitendo cha Marekani cha kuiba ndege yake
Feb 13, 2024 08:21Serikali ya Venezuela imelaani vikali kitendo cha Marekani cha kuiba waziwazi ndege iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni moja la Venezuela.
-
Wananchi wa Ghana washerehekea kurejeshwa turathi zilizoibiwa na Marekani
Feb 12, 2024 01:07Wananchi wa Ghana wanaendelea kusherehekea hatua ya kurejeshwa nchini humo turathi za thamani zilizokuwa zimeibiwa zaidi ya karne moja na nusu iliyopita na askari wa mkoloni Muingereza na kuhifadhiwa Marekani.
-
Iran yaonya kuhusu uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Israel
Feb 09, 2024 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya vikali Marekani dhidi ya kuendelea kuiunga mkono Israel na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.