May 21, 2024 12:07 UTC
  • Russia: Jamii ya kimataifa iendelee kuzishinikiza Marekani na utawala wa Kizayuni

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa jamii ya kimataifa inapasa kuendeleza mashinikizo kwa Marekani na utawala wa Kizayuni.

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amebainisha haya katika radiamali yake kwa jinai za utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza kwa uungaji mkono wa Magharibi na Marekani tangu Oktoba mwaka jana (2023). 

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Vasily Nebenzya Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kwamba kuna ulazima kwa jamii ya kimataifa kuziwekea mashinikkizo Marekani na utawala ghasibu wa Kizayuni.

Amesema, utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari unaendelea mashambulizi dhidi ya Gaza, na inaonekana haiwezekani kufikia malengo yote yaliyotangazwa.

Vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapelestina wa Ukanda Gaza 

Vasily Nebenzya ameashiria kifurushi cha dola bilioni 26 msaada wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa: Utawala ghasibu wa Israel unapokea makombora na mabomu mapya kwa ajili ya kuangamiza maisha ya Wapalestina. 

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa hadi sasa Wapalestina elfu 35,562 wameuawa shahidi huko Ukanda wa Gaza na wengine 79,652 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mauaji ya kimbari ya Israel. 

Tags