-
UN: Vijiji vinachomwa na watu wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa halaiki kaskazini mwa Msumbiji
Feb 08, 2020 12:57Umoja wa Mataifa umesema, watu wanayakimbia makazi yao ili kujinusuru na wimbi la hujuma na mashambulio katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji ambako mashuhuda wamesema, raia wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa umati huku vijiji vya eneo hilo vikiteketezwa kwa moto.
-
Rais Nyusi wa Msumbiji aapishwa, upinzani wasusia
Jan 16, 2020 02:32Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji alikula kiapo cha kulitumikia taifa jana Jumatano katika hafla iliyosusiwa na viongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo, wanaosisitiza kuwa kuliwepo na udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka uliomalizika wa 2019.
-
Mahakama Msumbiji yapinga rufaa ya wapinzani kuhusu matokeo ya uchaguzi
Nov 15, 2019 13:51Mahakama ya Katiba Msumbiji imetupilia mbali rufaa ya chama cha upinzani cha Renamo ambacho kilikuwa kinataka kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.
-
Upinzani Msumbiji wakataa kukubali matokeo ya uchaguzi
Oct 20, 2019 07:27Chama kikuu cha upinzani cha Renamo nchini Msumbiji kimepinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne iliyopita.
-
Wamsumbiji washiriki katika uchaguzi muhimu kwa amani na usalama wa nchi yao
Oct 15, 2019 08:04Wananchi wa Msumbiji leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura kushiriki katika uchaguzi unaotazamiwa kupima mafanikio ya makubaliano tete ya amani yaliyosainiwa miezi miwili iliyopita kati ya chama tawala cha Frelimo na hasimu wake wa vita vya muda mrefu vya ndani Renamo, ambayo sasa ni chama cha siasa cha upinzani.
-
UNICEF: Watoto milioni moja wanakabiliwa na hatari ya kifo nchini Msumbiji
Sep 18, 2019 07:50Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto milioni moja nchini Msumbiji wanakabiliwa na hatari ya kifo baada ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga.
-
Watu 10 wafariki, 98 wajeruhiwa kwenye msongamano wa kampeni za uchaguzi Msumbiji
Sep 13, 2019 07:23Watu wasiopungua 10 wamefariki dunia nchini Msumbiji na wengine 98 wamejeruhiwa katika vurugu na msongamano uliotokea katika mkutano wa kampeni za uchaguzi uliohutubiwa na rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi.
-
Rais wa Msumbiji na kiongozi wa Renamo wasaini makubaliano ya amani
Aug 02, 2019 01:20Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na Ossufo Momade, kiongozi wa Renamo, iliyokuwa harakati ya waasi na ambayo sasa ni chama cha siasa cha upinzani, wamesaini mkataba wa amani wa kuhitimisha uhasama wa vita vya kijeshi.
-
Wafadhili waahidi dola bilioni 1.2 kuisaidia Msumbuji baada ya vimbunga
Jun 03, 2019 03:42Jumla ya dola bilioni 1.2 zimechangishwa mjini Beira katika mkutano wa kimataifa wa siku mbili wa ufadhili kwa ajili ya ujenzi mpya wa kijamii, uzalishaji na miundombinu nchini Msumbiji baada ya taifa hilo kuathirika vibaya na vimbunga mapema mwaka huu.
-
Watu 16 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Msumbiji
Jun 01, 2019 11:22Kwa akali watu 16 wameuawa katika shambulizi jipya la kigaidi lililotokea huko kaskazini mwa Msumbiji.