-
Mgogoro wa Sudan na Misri wapanuka zaidi
Dec 26, 2017 23:14Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imeuandikia barua ya wazi Umoja wa Mataifa ikitangaza upinzani wake dhidi ya kile kilichotajwa kuwa ni makubaliano ya kuainisha mipaka ya nchi kavu kati ya Saudi Arabia na Misri.
-
Uturuki na Sudan zakubaliana kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili
Dec 25, 2017 11:26Uturuki na Sudan zimekubaliana kuanzisha baraza la ushirikiano wa kistratejia na kuzidisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi mbili hizo kufuatia ziara ya kihistoria iliyofanywa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Khartoum.
-
Mahasimu Sudan Kusini watia saini mapatano ya usitishaji vita
Dec 22, 2017 03:18Serikali ya Sudan Kusini imetiliana saini mapatano ya usitishaji vita na makundi ya waasi nchini humo jana Alkhamisi katika jitihada za hivi karibuni za kumaliza vita vya ndani ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka minne nchini humo.
-
Sudan, Rwanda kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi barani Afrika
Dec 22, 2017 03:13Sudan na Rwanda zimekubaliana kuunganisha juhudi zao za kutafuta suluhisho la amani la changamoto zinazolikabili bara la Afrika na kupambana na ugaidi na uhalifu wa kuchupa mpaka.
-
Sudan: Hatutaitambua mipaka mipya ya majini iliyowekwa na Misri na Saudia
Dec 21, 2017 12:47Sudan imewasilisha taarifa kwa Umoja wa Mataifa ikieleza kwamba endapo mipaka mipya ya majini iliyowekwa na Misri na Saudi Arabia itapitishwa rasmi haitoitambua katu mipaka hiyo.
-
AU kuanzisha tena juhudi za usuluhishi kati ya serikali ya Sudan na waasi wa eneo la Darfur
Dec 20, 2017 23:13Umoja wa Afrika utaanzisha tena usuluhishi kwa njia ya mazungumzo kati ya serikali ya Sudan na waasi wa Darfur baada ya mazungumzo hayo kusimama kwa muda wa miezi 16.
-
ICC yazijia juu nchi wanachama kwa kutomkamata Rais wa Sudan
Dec 13, 2017 23:42Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amezikosoa vikali baadhi ya nchi wanachama wa Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo, kwa kukataa kumtia mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan alipozitembelea.
-
ICC kuishitaki Jordan kwa kukataa kumtia nguvuni Rais wa Sudan
Dec 11, 2017 23:06Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza kuwa itairipoti Jordan katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kukataa kumtia nguvuni Rais Omar al-Bashir wa Sudan alipokuwa safari nchini humo mwezi Machi mwaka huu.
-
Wanajeshi 10 wa Sudan wauawa katika mapigano huko Darfur
Nov 28, 2017 04:17Askari 10 akiwemo kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Sudan wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka hivi karibuni katika jimbo la Darfur.
-
Kamanda wa kundi moja la waasi atiwa mbaroni Darfur Sudan
Nov 27, 2017 11:45Wizara ya Ulinzi ya Sudan imetangaza habari ya kutiwa mbaroni kamanda wa kundi moja la waasi wa eneo la Darfur la magharibi mwa Sudan kwa tuhuma za kuvunja haki za binadamu.