-
Kutangazwa muda wa kujiuzulu Rais Omar al Bashir wa Sudan
Aug 22, 2016 03:32Rais Omar al Bashir wa Sudan ametangaza kuwa, ana nia ya kuachia madaraka ifikapo mwaka 2020. Amesema atalazimika kuachana na siasa kwani katiba ya Sudan haitomruhusu kubakia madarakani.
-
Sudan kuanza mazungumzo ya usitishaji vita
Aug 10, 2016 03:27Mazungumzo yenye lengo la kufanikisha usitishaji vita wa kudumu katika mikoa mitatu ya Sudan iliyoathiriwa na mapigano yameanza Jumanne wiki hii siku moja baada ya muungano wa upinzani kusaini ramani ya njia ili kuhitimisha uhasama na kufikia suluhu ya kisiasa.
-
Rais wa ICC atakiwa kujiuzulu kwa kupokea rushwa ili 'kumshtaki al-Bashir'
Jul 27, 2016 02:52Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC anakabiliwa na mashinikizo ya kila upande ya kutaka ajiuzulu ili kupisha uchunguzi huru wa madai ya ufisadi wa kifedha dhidi yake katika kesi dhidi ya Rais wa Sudan Omar al-Bashir.
-
Rwanda: Hatutamkamata Rais al-Bashir wa Sudan akija nchini
Jul 14, 2016 23:42Rwanda imesema itamkaribisha Rais Omar al-Bashir wa Sudan atakapoizuru nchi hiyo kesho Jumamosi kuhudhuria kongamano Umoja wa Afrika AU, licha ya kiongozi huyo kuandamwa na waranti wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kutaka akamatwe.
-
Sudan: Kuongezwa muda vikosi vya UNAMID ni mkinzano
Jul 01, 2016 03:29Kwa mara nyingine tena serikali ya Sudan imekosoa vikali hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa kuhudumu vikosi vya kimataifa vya kusimamia amani huko Daruf UNAMID kwa mwaka mmoja zaidi.
-
Wasudan wakasirishwa na kupewa Saudia ardhi ya nchi yao
Jun 23, 2016 11:23Kitendo cha bunge la Sudan cha kupasisha makubaliano ya Khartoum na Riyadh ya kupewa Saudi Arabia haki ya kutumia hekari laki moja za ardhi ya kaskazini mwa Sudan, kimelalamikiwa vikali na wananchi wa nchi hiyo.
-
Shambulio la watu wenye silaha kusini magharibi mwa Sudan
Jun 21, 2016 22:58Watu waliokuwa na silaha wamewaua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine baada ya kushambulia eneo moja kusini magharibi mwa Sudan.
-
Sudan yalalamikia hatua ya UN kuongeza muda wa UNAMID
Jun 20, 2016 02:32Sudan imemuita mkuu wa vikosi vya kimataifa vya kusimamia amani huko Daruf UNAMID, kulalamikia hatua ya kuongezewa muda wa kuhudumu vikosi hivyo vyenye askari 20,000 kutoka nchi 30 duniani.
-
Kuanza mazungumzo baina ya Sudan na Sudan Kusini
Jun 06, 2016 22:03Mazungumzo kati ya maafisa wa Sudan na Sudan Kusini yalianza tena jana Jumatatu ya tarehe 6 Juni katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
-
Wasiwasi wa UNHCR kuhusu kutimuliwa Waeritrea nchini Sudan
Jun 03, 2016 09:57Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi la UNHCR limesema, lina hofu kubwa na hatua y ahivi karibuni ya kutimuliwa raia wa Eritrea walioko Sudan.