Asasi za kiraia nchini Sudan zasisitizia kuendeleza maandamano dhidi ya serikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19915-asasi_za_kiraia_nchini_sudan_zasisitizia_kuendeleza_maandamano_dhidi_ya_serikali
Asasi za kiraia nchini Sudan, zimesisitizia kuendeleza maandamano dhidi ya serikali juu ya siasa zake mbovu katika kupandisha bei ya mafuta nchini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 21, 2016 10:57 UTC
  • Asasi za kiraia nchini Sudan zasisitizia kuendeleza maandamano dhidi ya serikali

Asasi za kiraia nchini Sudan, zimesisitizia kuendeleza maandamano dhidi ya serikali juu ya siasa zake mbovu katika kupandisha bei ya mafuta nchini.

Taarifa iliyotolewa leo na asasi hizo imesisitiza kuwa, kamwe wananchi hawatokubaliana na maamuzi mapya ya serikali  na badala yake zitaendeleza juhudi zake za kumlazimisha Rais Omar al-Bashir wa nchi hiyo aangalie upya suala hilo la kuongeza bei ya nishati hiyo muhimu.

Maandamano ya wanawake wa Sudan

Wakati huo huo, mamia ya wanawake wa Sudan wamemiminika mabarabarani katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum wakiitaka serikali kuheshimu matakwa ya walio wengi na kusimamisha utekelezwaji wa siasa zisizo sahihi kuhusiana na uchumi. Miji ya Atbara na Niyalah, katikati mwa mkoa wa Darfur Kusini, ni kati ya maeneo yaliyoshuhudia maandamano kulalamikia siasa za uchumi za serikali ya Sudan.

Maandamano nchini Sudan

Maandamano hayo dhidi ya serikali yanazidi kushika kasi katika hali ambayo, maelfu ya raia wa taifa hilo wametaka kukomeshwa mpango wa kutekelezwa siasa za kubana matumizi sanjari na kufanyika marekebisho ya kiutawala.