Mgomo wa nchi nzima waanza Sudan kulalamikia bei ya mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20368-mgomo_wa_nchi_nzima_waanza_sudan_kulalamikia_bei_ya_mafuta
Mgomo wa nchi nzima kulalamikia kupungua kwa ruzuku ya mafuta kulikopelekea kupanda kwa bei ya nishati hiyo, umeanza leo nchini Sudan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 28, 2016 12:27 UTC
  • Mgomo wa nchi nzima waanza Sudan kulalamikia bei ya mafuta

Mgomo wa nchi nzima kulalamikia kupungua kwa ruzuku ya mafuta kulikopelekea kupanda kwa bei ya nishati hiyo, umeanza leo nchini Sudan.

Sekta mbalimbali kama vile usafirishaji na huduma nyingine za umma zimejiunga katika mgomo kulalamikia uamuzi wa serikali ya Khartoum wa kupunguza ruzuku ya mafuta, suala ambalo limeibua wimbi la malalamiko na maandamano nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vyombo vya usafirishaji kama mabasi vimesitisha huduma huku maduka na hoteli nazo zikifungwa kufuatia mgomo huo. Ripoti zaidi zinaelezea uwezekano wa kuibuka machafuko baina ya askari na wananchi.  

Wito wa kufanyika mgomo huo wa nchi nzima ulitolewa siku tatu zilizopita kupinga uamuzi wa serikali ya Sudan wa kupandisha kwa asilimia 30 nishati ya mafuta na gesi. Ongezeko hilo limepelekea pia kupanda kwa bei za bidhaa kama vyakula na madawa na hivyo kusababisha ughali zaidi wa maisha.