-
Viongozi wa Kiislamu Ulaya waanza safari ya kulaani ugaidi
Jul 08, 2017 22:22Makumi ya viongozi wa kidini na maimamu wa Swala za jamaa barani Ulaya wameanza safari ya kutembelea nchi kadhaa za bara hilo wakitokea mtaa mashuhuri wa Champs-Elysees mjini Paris. Viongozi hao wa kidini watatembelea maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi ya kigaidi katika miezi ya hivi karibuni.
-
Kukombolewa Benghazi, Khalifa Haftar azidi kujiimarisha
Jul 07, 2017 22:20Kukombolewa Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa wa Libya ambao umekuwa ukikaliwa na makundi ya kigaidi kwa kipindi cha miaka mitatu kumetajwa kuwa huenda kukaimarisha zaidi nafasi na Jenerali Khalifa Haftar na kumkurubisha zaidi kwenye udhibiti na madaraka ya Libya.
-
Hamaki za Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia baada ya kukwama siasa zao dhidi ya Qatar
Jul 07, 2017 01:33Adil al Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia ameshindwa kuzuia hamaki zake baada ya Qatar kukataa masharti ya nchi nne za Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Imarati na amedai mbele ya waandishi wa habari mjini Cairo Misri kwamba eti uuganji mkono wa Iran kwa Qatar ni kuunga mkono ugaidi.
-
Al Shabab waua Polisi 2 katika hujuma huko Lamu, Kenya
Jul 05, 2017 10:08Maafisa wawili wa polisi nchini Kenya wameuawa baada ya magaidi wanaoaminika kuwa wa kundi la Al Shabab kushambulia kituo cha polisi katika eneo la Pandanguo katika Kaunti ya Lamu.
-
Israel; hatari kuu ya ulimwengu wa Kiislamu
Jun 28, 2017 23:42Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ndiyo hatari kuu kwa umma wa Kiislamu na kwamba kitendo cha baadhi ya nchi za Kiislamu cha kuwa na uhusiano na Israel ni hatari kubwa kwa Waislamu.
-
Amani ya kudumu hupatikana kwa ushirikiano si kwa misimamo ya Kidaesh
Jun 27, 2017 08:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, eneo la Ghuba ya Uajemi limekumbwa na matatizo mawili makuu ya kimuundo na kutojitambua. Amesema, baadhi ya nchi za eneo hili zinaona usalama wao utapatikana kwa kununua amani kutoka nje wakati ambapo usalama wa kweli unaweza kupatikana tu kwa ushirikiano wa kieneo na kupitia nchi zenyewe za eneo hili.
-
Watu 15 wauawa katika hujuma ya al-Shabab mjini Mogadishu, Somalia
Jun 20, 2017 09:09Watu wasiopungua 15 wameuawa katika hujuma ya kigaidi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia huku kundi la kigaidi la al-Shabab likitangaza kuhusika na shambulizi hilo.
-
Kichapo cha makombora ya Iran kwa magaidi wa Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor, Syria
Jun 20, 2017 01:49Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) Jumapili usiku lilishambulia kwa makombora sita ya masafa ya kati ya ardhini kwa ardhini kamandi ya kijeshi ya magaidi wa kitakfiri wa Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor mashariki mwa Syria.
-
Putin: Marekani inatumia ugaidi kama wenzo
Jun 14, 2017 21:59Huku mivutano kati ya Moscow na Washington ikiwa imepamba moto, Rais Vladimir Putin wa Russia amesisitiza kuwa, Marekani inawaunga mkono magaidi wa Chechniya huko Kaukazia Kaskazini na kuwatumia magaidi hao kuvuruga usalama na utilivu wa Russia. Rais Putin amesema Idara za Intelijensia za Marekani zimewapa misaada ya kiintelijensia, kisiasa, kifedha na kadhalika magaidi Chechniya licha ya malalamiko na upinzani wa Moscow.
-
Rouhani: Iran daima imekuwa mstari wa mbele kupambana na ugaidi
Jun 13, 2017 23:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini, Iran ilikabiliana na wimbi la ugaidi na kupoteza maelfu ya mashahidi, na kwamba daima imekuwa mstari wa mbele kupambana na ugaidi.