-
Umoja wa Mataifa walaani matamshi ya kibaguzi ya Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni
Oct 26, 2016 01:09Umoja wa Mataifa umelaani matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba anakusudia yeye mwenyewe binafsi kushiriki katika uchimbaji mashimo chini ya msikiti wa Al- Aqsa.
-
UN: DAESH wamewaua kinyama raia wengi wa mji wa Mosul
Oct 26, 2016 01:08Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umepokea ripoti kadhaa zinazoonyesha kuwa, sambamba na vikosi vya jeshi la Iraq kukaribia mji wa Mosul kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limeua makumi ya watu wakiwemo maafisa 50 wa polisi ya Iraq ambao wameuliwa kinyama na magaidi wa kundi hilo.
-
Askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa CAR walaumiwa kwa udhaifu
Oct 25, 2016 02:29Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekosoa vikali udhaifu wa askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa ndani ya nchi hiyo.
-
UN: Mabinti elfu 47 katika hatari ya kulazimishwa ndoa za mapema kila siku
Oct 22, 2016 00:56Umoja wa Mataifa umeonya kuwa, watoto wadogo wa kike zaidi ya elfu 47 wapo katika hatari ya kulazimishwa kushiriki ndoa za mapema kila siku duniani.
-
Syria: Magaidi wanazuia raia kutoka mji wa Aleppo
Oct 21, 2016 10:23Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wanawazuia raia kuugura mji wa Aleppo, ambao kwa sasa unashuhudia makabiliano makali kati ya vikosi vya serikali na magenge ya kigaidi.
-
UN yaeleza matumaini yake kuhusu makubaliano ya kisiasa DRC
Oct 20, 2016 10:18Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema ana wingi wa matumaini kuwa makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa Jumanne iliyopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yatasaidia kuheshimiwa haki za binadamu sambamba na kufanyika uchaguzi wenye itibari katika nchi hiyo ya Kiafrika.
-
UN: Hali ya hatari Ethiopia inalenga wanadiplomasia na wanahabari
Oct 18, 2016 03:34Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema anafuatilia kwa karibu matukio ya hivi sasa nchini Ethiopia na kueleza wasi wasi wake kuwa hali ya hatari iliyotangazwa hivi karibuni na serikali ya Addis Ababa, inawaathiri zaidi wanadiplomasia na waandishi wa habari.
-
Ansarullah: Umoja wa Mataifa uchunguze ukatili wa Saudia Yemen
Oct 17, 2016 00:58Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa juu ya mauaji ya kinyama yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia nchini Yemen hivi karibuni.
-
UN yalaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
Oct 15, 2016 04:40Kikao maalumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimekosoa vikali kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na utawala ghasibu wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
UN yalaani kutumiwa mabavu dhidi ya raia Jamhuri ya Afrika ya Kati
Oct 14, 2016 11:37Umoja wa Mataifa umelaani kuuliwa raia katika machafuko mapya ya makundi yenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.