-
Burujerdi amtaka Ban Ki-moon kuiweka tena Saudia katika orodha yake nyeusi
Jun 12, 2016 09:43Mwakilishi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapasa kwa mara nyingine tena kuchukua hatua ya kijasiri na kuliweka jina la Saudi Arabia katika orodha nyeusi ya Umoja huo kwa kukiuka haki za watoto.
-
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Jun 12, 2016 09:02Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu imetoa ripoti inayoeleza kuwa Israel imeua Wapalestina 53 tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016.
-
Polisi wa Burundi kuondolewa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jun 12, 2016 00:00Umoja wa Mataifa umetangaza habari ya kuondolewa maafisa wa polisi wa Burundi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao wa Julai.
-
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa laazimia kuangamiza Ukimwi Duniani
Jun 11, 2016 10:59Mkutano wa ngazi ya juu wa siku tatu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu namna ya kukomesha maambukizi ya Ukimwi umefungwa mjini New York.
-
UN yalaani matamshi ya chuki za kikabila ya Rais wa Gambia
Jun 11, 2016 10:59Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Uzuiaji Mauaji ya Kimbari amelaani hotuba ya kichochezi ya Rais Yahya Jammeh wa Gambia ya kutishia kuliangamiza kabila la Mandinka nchini humo.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aikosoa Saudia
Jun 09, 2016 23:16Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashinikizo yanayotolewa na Saudia kuhusu hatua yake ya kukiuka haki za watoto huko Yemen ni jambo lisiloweza kuhalalishwa.
-
Kuteuliwa utawala wa Kizayuni kuongoza kamati ya sheria ya Umoja wa Mataifa
Jun 09, 2016 02:30Harakati kubwa zilizofanywa kuupatia utawala wa Kizayuni wa Israel uwanachama kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kuupatia uongozi utawala huo kwenye baraza hilo ambako kumeonyesha ufanyaji mkubwa wa mambo kisiasa na upotoshaji malengo na vigezo vya kisheria katika chombo hicho cha kisheria cha UN, vimezidi kudhihirisha jinsi suala la haki za binadamu linavyoendelea kutumiwa kisiasa.
-
Palestina: Ni kinaya kuteuliwa Israel kuongoza kamati ya UN
Jun 08, 2016 23:12Afisa wa ngazi za juu wa Palestina ameitaja kama kichekesho na kinaya, hatua ya kuteuliwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa.
-
Umoja wa Mataifa wataka viongozi wa Eritrea wapelekwe ICC
Jun 08, 2016 09:44Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwekewa vikwazo na kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC viongozi na wanasiasa wa Eritrea, kwa tuhuma za kufanya jinai dhidi ya binadamu.
-
Saudia yatishia kuikatia UN ufadhili kwa kuiweka kwenye orodha nyeusi
Jun 08, 2016 08:46Saudi Arabia imetishia kukata misaada na ufadhili wake kwa Umoja wa Mataifa, siku chache baada ya Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa umoja huo kuuweka muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na nchi hiyo dhidi ya Yemen kwenye orodha yake nyeusi.