Mogherini: Mpango wa JCPOA uko katika mkondo sahihi
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i3163-mogherini_mpango_wa_jcpoa_uko_katika_mkondo_sahihi
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ametangaza katika ripoti aliyotoa baada ya kufanyika kikao cha mashauriano kati yake na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwa utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) upo katika mkondo sahihi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 16, 2016 03:45 UTC
  • Mogherini: Mpango wa JCPOA uko katika mkondo sahihi

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ametangaza katika ripoti aliyotoa baada ya kufanyika kikao cha mashauriano kati yake na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwa utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) upo katika mkondo sahihi.

Bi Federica Mogherini ametangaza kwenye ripoti hiyo kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) katika ripoti uliyotoa hivi karibuni, umethibitisha rasmi kwamba Iran imetekeleza ahadi zake zote.

Mogherini ameashiria pia kufanyika uchaguzi siku kadhaa zilizopita hapa nchini na kubainisha kuwa: Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha wazi imani ya wananchi wa Iran kwa mpango wa marekebisho ya kiuchumi ya Rais wa Iran.

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema ana mpango wa kufanya ziara nchini Iran tarehe 16 mwezii Aprili mwaka huu na kuongeza kuwa, katika safari yake hiyo ambapo atafuatana na makamishna wa nishati na hali ya hewa, utafiti, mazingira, mashirika na taasisi za ajira, masuala ya kibinadamu, elimu na usafirishaji wa Umoja wa Ulaya, watakuwa na mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali muhimu katika sekta ya biashara, uwekezaji, nishati n.k.