Al-Qassam: Tunaendelea kupambana na wavamizi katika medani kadhaa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103222-al_qassam_tunaendelea_kupambana_na_wavamizi_katika_medani_kadhaa
Msemaji wa Brigedi ya Al-Qassam amesisitiza kutumiwa makombora na wanamuqawama katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kubainisha kuwa wataendeleza vita dhidi ya utawala wa Kizayuni katika medani kadhaa.
(last modified 2026-07-28T12:43:49+00:00 )
Oct 08, 2023 10:07 UTC
  • Al-Qassam: Tunaendelea kupambana na wavamizi katika medani kadhaa

Msemaji wa Brigedi ya Al-Qassam amesisitiza kutumiwa makombora na wanamuqawama katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kubainisha kuwa wataendeleza vita dhidi ya utawala wa Kizayuni katika medani kadhaa.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imejibu hatua za uhasama na chokochoko za utawala wa Kizayuni ambapo tangu jana Jumamosi imevurumisha mamia ya makombora na roketi katika ardhi zinazozokaliwa kwa mabavu ikiwemo huko Tel Aviv, Ashdodi na Ashkeloni. 

Oparesheni za Kimbunga cha Al Aqsa na kutekwa kifaru cha wanajeshi wa Israel 

Hadi sasa zaidi ya Wazayuni 600 wameangamizwa katika mashambulizi hayo ya wanamuqawama wa Palestina, na wengine 1700 kujeruhiwa; ambapo hali za baadhi ya majeruhi ni mbaya sana. 

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa,  Abu Obeidah Msemaji wa Brigedi za al Qassam leo ametangaza kuwa na hapa ninamnukuu" Tunawaomba wananchi wetu washiriki katika medani zote katika vita hii ya aina yake katika historia."  

Abu Obeidah ameongeza kuwa: Kamandi ya al-Qassam iliweza kubadilisha idadi ya wanamuqawama katika kambi za kijeshi na  vikosi vingine, na kufanya operesheni mpya ya kujipenyeza ili kuwaunga mkono wanamapambano sambamba na kujizatiti kwa silaha katika medani kadhaa.  

Wakati huo huo, Kanali Richard Hatch Msemaji  wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni leo asubuhi alitangaza kuwa, askari 30 wa jeshi la utawala huo wameuawa na wapiganaji wa Hamas huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kwamba idadi ya Wazayuni waliouliwa hadi sasa ni 350.