WHO yatahadharisha kuhusu mfumo wa matibabu Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103430-who_yatahadharisha_kuhusu_mfumo_wa_matibabu_ukanda_wa_ghaza
Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa mfumo wa huduma za afya huko Ghaza unaelekea kusambaratika kufuatia mzingiro na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 13, 2023 07:49 UTC
  • WHO yatahadharisha kuhusu mfumo wa matibabu Ukanda wa Ghaza

Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa mfumo wa huduma za afya huko Ghaza unaelekea kusambaratika kufuatia mzingiro na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la SAMA la Palestina limeripotikuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa mfumo wa afya na matibabu huko Ghaza unakaribia kusambaratika na kusisitiza juu ya ulazima wa kutumwa haraka iwezekanavyo misaada ya kkitiba na afya kwa wakazi wa ukanda huko ili kuzuia maafa ya binadamu.  

Katika upande mwingine, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa hadi sasa Wapalestina 423,000 wamekuwa wakimbizi kufuatia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.  

Wizara ya Afya ya Ghaza pia awali iliripoti kuhusu kushtadi mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza na kueleza kuwa: Hadi sasa Wapalestina 1,537 wameuliwa shahidi na wengine 6,612 kujeruhiwa katika hujuma za kikatili za utawala haramu wa Israel.  

Wanamuqawama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya ya Palestina (Hamas) tangu tarehe 7 mwezi huu Oktoba wameanzisha oparesheni ya pande zote na ya aina yake kwa jina la "Kimbunga cha al Aqsa" kutokea Ukanda wa Ghaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. 

Utawala wa Kizayuni ambao umeshangazwa katika medani ya vita na muqawama wa Palestina kwa kushindwa kwa fedheha  siku chache zilizopita, umefunga vivuko vyote vya Ukanda wa Ghaza katika hatua yake isiyo ya kibinadamu ili kuulazimisha muqawama wa Palestina usimamishe operesheni ya kishujaa ya Kimbunga cha Al Aqsa.