Al Azhar yawataka Waislamu kukabiliana na adui Mzayuni
(last modified Wed, 18 Oct 2023 06:16:29 GMT )
Oct 18, 2023 06:16 UTC
  • Al Azhar yawataka Waislamu kukabiliana na adui Mzayuni

Chuo Kikuu cha Al Azhar cha nchini MIsri kimewataka Waislamu duniani kote kukabiliana kwa uwezo na nguvu zote na jinai za utawala wa Kizayuni.

Utawala wa Kizyauni jana usiku uliipiga kwa mabomu hospitali ya Maamadani huko Ghaza na hadi sasa Wapalestina zaidi ya 500 wameripotiiwa kuuliwa shahidi. 

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Chuo Kikuu cha Al Azhar Misri kimetangaza katika taarifa yake kuwa, Umma wa Kiislamu unapasa kutumia uwezo na utajiri wake wote na kila ulichonacho ili kuihami Palestina na kuwalinda wananchi madhulumu wanaokabiliwa na uadui wa kinyama wa utawala unaotenda jinai na usio na ubinadamu wala maadili. 

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri amelaani kushambuliwa kwa makusudi hospitali ya Maamadani katika Ukanda wa Ghaza na kusema hujuma hiyo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na ubinadamu. 

Amesisitiza juu ya msimamo wa serikali na wananchi wa Misri katika kulaani jinai hiyo dhidi ya raia na kutaka kusitishwa mara moja mashambulizi ya Israel huko Ghaza. 

Raia katika nchi mbalimbali za Kiislamu na za Kiarabu pia wamemiminika katika mitaa mbalimbali ya nchi zao kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. Wamezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza kuwa mfano wa wazi wa ukatili mkubwa unaotekelezwa katika karne ya 21.

Raia hao katika nchi mbalimbali za Kiislamu na Kiarabu aidha wamepiga nara na shaari za kudhihirisha hasira na kuchukuizwa kwao na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza; ambapo wamechoma moto bendera ya utawala wa Kizayuni na picha ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel. 

Maandamano nchini Iran dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza 

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepanga kuitisha kikao ili kuipigia kura rasimu ya azimio kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza. 

Hii ni katika hali ambayo kikao cha jana cha Baraza la Usalama cha kuchunguza na kuipigia kura rasimu ya azimio la kuulazimisha utawala wa Kizayuni unaouwa watoto usitishe mashambulizi yake Ukanda wa Ghaza kilimazika bila ya kupasishwa rasimu hiyo.