Israel imebomoa misikiti 56 kikamilifu katika vita dhidi ya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104524-israel_imebomoa_misikiti_56_kikamilifu_katika_vita_dhidi_ya_gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umeshambulia na kuharibu kabisa kwa mabomu misikiti 56 tokea unazish vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Gaza. Aidha misikiti mingine zaidi ya 192 imepata hasara kwa kuharibiwa katika mashambulizi hayo ya kinyama.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Nov 08, 2023 11:05 UTC
  • Israel imebomoa misikiti 56 kikamilifu katika vita dhidi ya Gaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umeshambulia na kuharibu kabisa kwa mabomu misikiti 56 tokea unazish vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Gaza. Aidha misikiti mingine zaidi ya 192 imepata hasara kwa kuharibiwa katika mashambulizi hayo ya kinyama.

Vyombo vya habari vya Gaza vinaripoti kuwa mashambulizi yanayoendelea ya utawala wa kivita dhidi ya Ukanda wa Gaza yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo lililozingirwa la Palestina.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza, Salama Marouf, tathmini ya uharibifu huo ni pamoja na uharibifu wa miundo msingi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maeneo ya ibada, vituo vya matibabu, taasisi za elimu na makazi ya raia..

Tarehe 20 Oktoba pia Wakristo wasiopungua 18 wa Kipalestina waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la anga la Israel lililolenga Kanisa hilo la Kiothodoksi la Ugiriki katika Ukanda wa Gaza.

Kanisa la Saint Porphyrius linalohesabiwa kuwa moja ya makanisa makongwe zaidi katika eneo, linapatikana katika eneo la Zeitoun, kusini mwa Gaza.

Hali baada ya ndege za kivita za Israel kudondosha mabomu katika eneo la Raia

Mbali na hayo, ripoti za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaonyesha ukweli wa kutisha: Karibu nusu ya majengo ya Gaza yameharibiwa au kubomoka kabisa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyoanza Oktoba 7. Mfumo wa huduma ya afya uko katika hali ya kuporomoka, huku zaidi ya theluthi moja ya hospitali zikiwa hazifanyi kazi na zilizosalia zina mgao wa mafuta, vifaa, nafasi na dawa.

Kupungua kwa kasi kwa asilimia 92 kwa matumizi ya maji safi ya mifereji kutoka viwango vya kabla ya migogoro kunaashiria kuanguka kwa mtandao wa usambazji maji uliokuwa ukifanya kazi. Aidha idadi kubwa ya vituo vya maji taka sasa havifanyi kazi, watu wa Gaza wanakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa maji na usafi wa mazingira ambapo mashirika ya kutoa misaada yanasema  uhaba huo sasa ni wa kiwango cha janga.