Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ametangaza kuwa: idadi ya askari na maafisa wa jeshi la utawala huo ghasibu waliouawa tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefika 351.
Wanajeshi wa Kizayuni walioangamizwa wafika 351, Muqawama wasisitiza kuwa hautashindwa
Nov 09, 2023 03:44 UTC
Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ametangaza kuwa: idadi ya askari na maafisa wa jeshi la utawala huo ghasibu waliouawa tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefika 351.
Kwa mujibu wa IRNA; Hagari aidha amesema, idadi ya watu aliodai kuwa walitekwa nyara na kupelekwa Ukanda wa Gaza (mateka wa Israel) ni watu 239.
Wakati huo huo, Saleh al-Aroori, naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema: "kadiri adui Mzayuni anavyozidi kupenya na kujiingiza ndani ya Gaza, ndivyo hasara na maafa yatakayowafika wanajeshi wake yatazidi kuongezeka."
Afisa huyo wa Hamas ameeleza bayana kuwa: "vita hivi vitakuwa na athari na matokeo kadhaa", na akasisitiza kwamba Muqawama hautashindwa.
Saleh al-Aroori
Al-Aroori aidha amebainisha kuwa, adui Mzayuni atajiondoa na kurudi nyuma kutoka Gaza kutokana na kuteketezwa vifaru vyake vingi zaidi na kuongezeka askari wake watakaouawa.
Kiongozi huyo wa Hamasa amesisitiza kuwa mpango wa adui wa kuwahamishia Misri watu wa Gaza na wakazi wa kaskazini kuelekea kusini haukufaulu na akaongezea kwa kusema: ni 25% tu ya wakazi wa maeneo ya kaskazini waliokwenda kusini.
Katika jibu ililotoa kwa madhila ya zaidi ya miongo saba ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na zaidi ya miaka kumi na tano ya kuwekewa mzingiro Gaza na kufungwa jela na kuteswa maelfu ya Wapalestina, mnamo tarehe 7 Oktoba, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
Operesheni hiyo inachukuliwa kuwa moja ya mashambulio makali zaidi dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni. Wapiganaji wa Hamas walipenya kwenye maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kupitia nukta kadhaa za uzio wa mpakani na kushambulia vijiji kadhaa, ambapo mbali na kuangamiza idadi kubwa ya Wazayuni, waliwakamata mateka wengine kadhaa miongoni mwao.../