Nasrullah: Upande ambao inapasa ukate tamaa ni wa utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104654-nasrullah_upande_ambao_inapasa_ukate_tamaa_ni_wa_utawala_wa_kizayuni
Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amesema, adui Mzayuni ameboronga tena katika mahesabu kama ilivyokuwa huko nyuma, na akasisitiza kwamba: wananchi wa Lebanon wameshikamana zaidi hivi sasa na Muqawama.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Nov 11, 2023 23:36 UTC
  • Nasrullah: Upande ambao inapasa ukate tamaa ni wa utawala wa Kizayuni

Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amesema, adui Mzayuni ameboronga tena katika mahesabu kama ilivyokuwa huko nyuma, na akasisitiza kwamba: wananchi wa Lebanon wameshikamana zaidi hivi sasa na Muqawama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IranPress, Sayyid Hassan Nasrullah amesema, inaonekana Wazayuni hawajapata funzo kutokana na mauaji, kuwahamisha kwa nguvu na kuwabomolea nyumba zao watu wa Palestina katika muda wa miaka 75 iliyopita na akahoji: "ni nini matokeo ya vitendo hivyo? Je, watu wa Palestina wameacha mapambano na muqawama? Kinyume chake, muqawama, irada na utamaduni huu vimeimarishwa kizazi baada ya kizazi, hadi kufikia kiwango cha juu kabisa mwaka huu na kufikia kwenye Kimbunga cha Al-Aqsa. Hali ni hiyo hiyo Lebanon. Baada ya mauaji yote yaliyofanywa na Wazayuni, wananchi wa Lebanon hawakuacha mapambano na muqawama".
 
Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongezea kwa kusema: "utawala wa Kizayuni unashambulia Ukanda wa Gaza dhahir shaihir, waziwazi na kwa namna ya kufedhehesha. Unyama wa Israel katika Ukanda wa Gaza haujapungua, bali unaongezeka kila siku. Mashambulizi haya yanaonyesha khulka ya kisasi cha kinyama cha Kizayuni ambacho hakina mpaka wowote.
Uharibifu wa majengo uliofanywa na jeshi la Kizayuni Gaza

Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, "adui Mzayuni ameboronga tena katika mahesabu kama ilivyokuwa huko nyuma, na akasisitiza kwamba: wananchi wa Lebanon wameshikamana zaidi hivi sasa na Muqawama. Lakini kwa bahati mbaya, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wa Kiarabu na wa Kimagharibi, kwa makusudi na wengine bila kukusudia wanafanya mambo kwa kufuata lengo la Wazayuni. Upande ambao inapasa ukate tamaa ni wa Israel; Israel itambue kuwa kutokana viwiliwili vya mashahidi wa Gaza na Lebanon, vitaibuka vizazi vya Muqawama ambavyo vitakuwa na azma imara zaidi ya kupambana naye na kumuangamiza ghasibu huyo.

 
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema damu ya mashahidi imekuwa kigingi na kizuizi dhidi ya maadui na akaongeza kuwa : Mashahidi wetu wana maono na basira. Wanamjua rafiki na adui na njia sahihi na potofu. Wao wanajua nini cha kufanya katika wakati na mahala mwafaka. Wanawajibika na ni watu wa matendo, jihadi na subira.../