Al Mayadeen: Israel inazuia misaada ya kibinadamu ya Iran kuingia Gaza
Katika hali ambayo Wapalestina wanahitaji sana dawa na vifaa vya matibabu, televisheni ya Al-Mayadeen imeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni haujaruhusu misaada ya kibinadamu ya Iran kuingia Gaza kupitia Misri.
Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, televisheni ya al Mayadeen imezinukiuu duru kadhaa za kisiasa na kuripoti kuwa utawala wa Kizayuni haujaruhusu misaada ya kibinadamu ya Iran kuingia Ukanda wa Gaza kupitia Misri.
Al Mayadeen imeandika kuhusiana na suala hili kwamba: Misri imeoamba radhi kufuatia hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kupinga kuingia Ukanda wa Gaza misaada hiyo ya kibinadamu ya Iran kupitia kivuko cha Rafah.
Utawala wa Kizayuni umepinga kuingia Gaza misaada ya kibinadamu ya Iran katika hali ambayo viongozi wa utawala huo haramu umeruhusu baadhi ya misaada kuingiza Ukanda wa Gaza baada tu ya kukagua shehena mbalimbali za misaada ya kibinadamu iliyotumwa na ncxhi mbalimbali na tena kwa kucheleweshwa kwa masaa kadhaa.
Hospitali na vituo kadhaa vya tiba huko Ukanda wa Gaza siku kadhaa zilizopita ziliishiwa na akiba ya mafuta na kutangaza kuwa zinahitaji haraka suhula na vifaa tiba; ambapo hadi sasa utawala Kizayuni umezuia kuingia Gaza misaada mingi iliyotumwa kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Oktoba mwaka huu Iran ilituma Misri tani 60 za misaada mbalimbali ya kibinadamu ili misaada hiyo iweze kufika Gaza kupitia nchi hiyo. Shehena za misaada ya Iran iliyojumuisha bidhaa mbalimbali za chakuka, vifaa tiba na dawa ilitumwa katika uwanja wa ndege wa al Arish huko Misri baadaya kufanyika uratibu na mawasiliano yaliyohitajika.
Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alizungumza na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku za awali za kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Ukanda wa Gaza ambapo alisema Iran iko tayari kutuma misaada ya kibinadamu Ukanda wa Gaza.