Wazayuni wakiri: Helikopta yetu wenyewe ilishambulia walowezi katika tamasha la muziki
Baada ya kupita zaidi ya mwezi mmoja, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwa helikopta yake iliwalenga kimakosa walowezi waliokuwepo kwenye tamasha la muziki karibu na Ukanda wa Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba.
Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA, gazeti la Kizayuni la Ha'aretz, limenukuu ripoti ya uchunguzi wa polisi ya utawala wa Kizayuni na kuandika kuwa mnamo tarehe 7 Oktoba, helikopta ya kijeshi ya Israel iliwaua kimakosa watu kadhaa waliohudhuria tamasha karibu na kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Rayim.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, akthari ya waliohudhuria tamasha hilo walifanikiwa kukimbia.
Katika sehemu nyingine ya uchunguzi huo imeelezwa kuwa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS haikuwa ikijua chochote kuhusu kufanyika kwa tamasha hilo.
Ikumbukwe kuwa tangu ilipoanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba, vyombo vya habari na maafisa wa utawala wa Kizayuni wamekuwa wakidai kuwa, vikosi vya Hamas viliwashambulia na kuwaua waliohudhuria tamasha hilo kwa lengo la kukuza maafa ya tukio hilo na kujenga taswira bandia na ya uwongo ya kuuonyesha utawala huo dhalimu kuwa ni mdhulumiwa.
Utawala ghasibu wa Kizayuni ulilitumia shambulio hilo dhidi ya tamasha hilo la muziki kama kisingizio cha kuanzisha mashambulio ya kila upande dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza na ukapata uungaji mkono na baraka kamili za nchi za Magharibi hususan Marekani za kufanya mauaji ya kikatili na ya umati dhidi ya Wapalestina.
Kwa upande mwingine, chaneli ya habari ya CNN imeandika katika uchambuzi wake kwamba kuna uwezekano jeshi lenyewe la Israel liliweka silaha katika hospitali ya Al-Shifaa kabla ya kuwasili timu za vyombo vya habari.
CNN imeandika, video iliyotolewa na jeshi la Israel mnamo Novemba 15, ya kuonyesha kwamba lilikuta silaha za Hamas katika hospitali ya Al-Shifaa inaonyesha silaha chache kwenye eneo la tukio kuinganisha na video zilizorekodiwa baadaye na timu za vyombo vya habari vya kimataifa. Hii inaonyesha kuwa silaha hizo zinaweza kuwa zilihamishwa au kuwekwa hapo kabla ya kufika timu za vyombo vya habari za kimataifa.
Kabla ya hapo, Hamas ilishatahadharisha kuhusu uwezekano wa utawala wa Kizayuni kuandaa na kuweka silaha katika Hospitali ya Al-Shifaa ili kuhalalisha jinai zake na kuelekeza tuhuma kwa Muqawama.../