Ujumbe wa Hamas umeondoka Cairo kwa ajili ya mashauriano zaidi
(last modified Tue, 30 Apr 2024 11:12:39 GMT )
Apr 30, 2024 11:12 UTC
  • Ujumbe wa Hamas umeondoka Cairo kwa ajili ya mashauriano zaidi

Ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) umeondoka Cairo, mji mkuu wa Misri ili kufanya mashauriano zaidi kuhusu pendekezo jipya lililotolewa kwa ajili ya kubadilishana mateka.

Shirika la habari la Palestina la SAMA mapema leo limeripoti kuwa, ujumbe wa harakati ya Hamas umeondoka Cairo baada ya kupokea pendekezo jipya kuhusu kubadilishana mateka na kuzungumza chini ya upatanishi wa Misri na Qatar na kupokea ushauri wa pande hizo. Ujumbe wa Hamas utarejea Cairo na majibu ya maandishi kwa pendekezo la kusitisha vita huko Ukanda wa Gaza.  

Ujumbe wa Hamas waondoka Cairo 

Ihsan Ataya mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema kuwa pendekezo hilo haliwezi kupelekea kusimamishwa vita Ukanda wa Gaza kutokana vipengee na utata wa pendekezo hilo. 

Gazeti la Hume la Israel limedai kuwa utawala wa Kizayuni uko tayari kukubali masharti ya Hamas ili kusimamisha vita na kujibu matakwa yote ya harakati hiyo isipokuwa kutangaza kuhitimisha vita baada ya duru ya kubadilishana mateka. 

Gazeti hilo la Israel limeandika kuwa: Israel inapanga kutenga siku 10 hadi wiki 2 kufikia makubaliano na Hamas ili kuwaachilia huru idadi ya mateka wa Israel.