Ansarullah: Tumeshambulia meli 170 zilizokuwa zikielekea Israel
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza kuwa, idadi ya meli zilizoshambuuliwa na ambazo zinazohusiana na meli za Marekani, Israel na Uingereza katika Bahari Nyekundu zilizokuwa zikielekea katika bandari za ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina imefikia meli 170.
Seyyed Abdul Malik al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, operesheni za kambi ya Yemen dhidi ya meli zinazoelekea katika bandari za ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) zilitekelezwa tena wiki hii kwa makombora 25 ya balistiki, ndege zisizo na rubani na boti za jeshi la wanamaji.
Seyed al-Houthi amesisitiza kuwa, taathira za kiuchumi kwa adui Israel zimefikia bayana hadi adui akatangaza kufilisika bandari ya Umm al-Rasrash (Eilat) ambayo ilikuwa ni chanzo kikubwa cha mapato katika masuala ya fedha na kiuchumi na shughuli za kibiashara.
Kiongozii huyo wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kuwa, mamlaka za utawala ghasibu wa Israel zimekiri kwamba ziko katika njia panda ya kihistoria na yanayojiri kaskazini mwa Palestina ni kushindwa vibaya zaidi tangu mwaka 1948 katika eneo hili.
Yemen imetuma ilani rasmi kwa mashirika ya bima duniani na kutangaza kuwa meli ambazo zote zinamilikiwa na watu binafsi wanaohusishwa na Israel au mashirika ya utawala wa Israel; Meli zenye bendera ya Israel, au zile zinazomilikiwa na watu au mashirika ya Marekani au Uingereza, au kusafiri chini ya bendera za Marekani au Uingereza, zimepigwa marufuku kupita Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia.