Rais Maduro: Venezuela daima itakuwa pamoja na wananchi wa Palestina
(last modified Sun, 04 Aug 2024 12:15:48 GMT )
Aug 04, 2024 12:15 UTC
  • Rais Maduro: Venezuela daima itakuwa pamoja na wananchi wa Palestina

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amelaani mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, nchi hiyo ya Amerika ya latini daima itakuwa pamoja na Palestina.

Rais Maduro amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kwamba, nguvu na haki ya kuishi na mustakabali wa taifa la Palestina utapatikana kwa kuvuka matatizo ya sasa.

Amesema, serikali ya Caracas inaunga mkono muqawama na mapambano ya Palestina ambayo yatapata ushindi kwa kuchelewa au kwa haraka.

Maduro ameongeza kuwa, zaidi ya wakimbizi milioni moja na nusu wa Kipalestina kote duniani na Venezuela daima imekuwa ikiunga mkono haki ya wananchi wa Palestina kurejea katika ardhi yao na kupata amani na uhuru wao.

 

Vita vya maangamizi ya umati vya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza vilianza baada ya Harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas kutekkeleza Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqswa mnamo Oktoba 7 ili kukabiliana na miongo kadhaa ya uhalifu na jinai za utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Zaidi ya Wapalestina 39,000 wameuawa shahidi huku wahanga wakuu wa jinai hizo za utawala haramu wa Israel huko Gaza wakiwa ni wanawake na watoto. Aidha jeshi la Israel limebomoa mamia ya shule, hospitali na misikiti na kuharibu miundombinu ya Ukanda huo.

Tags