Oct 03, 2024 11:14 UTC
  • Kuna tofauti kubwa baina ya Mayahudi na Wazayuni (PICHA)

Katika kujibu swali linalosema kuwa, je, kuna tofauti baina ya Mayahudi na Wazayuni, tunapenda kusema kwamba, naam, kuna tofauti kubwa baina ya makundi hayo mawili.

Hapa chini pamoja na maelezo machache, tutajibu swali hilo kwa sura ya picha. Lakini kwanza tunasema kwamba, Waislamu, Wakristo na Mayahudi walikuwa wakiishi kwa salama kwa karne nyingi katika ardhi za Palestina kabla ya kuzuka donda ndugu la Uzayuni. 

Wakati Waislamu walipokuwa wanatawala Palestina, hakukuwa na ukandamizaji wowote dhidi ya Mayahudi wala Wakristo. Mgogoro mkubwa ulianza baada ya wakoloni wa Uingereza kupandikiza donda ndugu la kensa liitwalo Uzayuni katika ardhi takatifu za Waislamu, Wakristo na Mayahudi huko Palestina. 

Wakati Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapoendesha mapambano na Muqawama wa pande zote na kuvumilia shida na matatizo yasiyo na idadi kwa karibu miaka 50 sasa, katika mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Wazayuni, muda wote imekuwa ikichunga kikamilifu uhakika huo kwamba kuna tofauti kubwa baina ya Mayahudi na Wazayuni.

Mtu anaweza kuwa ni Myahudi, lakini si Mzayuni na mtu anaweza kuwa si Myahudi lakini ni Mzayuni kwani Uzayuni ni fikra chafu iliyojengeka juu ya msingi wa dhulma, ukatili na kutokuwa na ubinadamu hata chembe. 

Picha ya kihistoria inayoonesha Mayahudi wakiwasili Palestina kutokea Ulaya mwaka 1947
Kuna tofauti kubwa baina ya Mayahudi na Wazayuni, hapa Mayahudi wanaonekana wakichoma moto bendera ya dola pandikizi la Kizayuni
Mayahudi nchini Iran wana uhuru kamili wa kufanya ibada na sherehe zao kwa bila ya kubugudhiwa
Sasa hawa ndio Wazayuni, hapa wanaendeleza ukandamizaji na unyanyasaji wao dhidi ya Waislamu wa Palestina bila ya kujali umri wala jinsia zao
Wazayuni hawana chembe ya utu. Ukatili wao huko Palestina hasa dhidi ya wananchi wa Ghaza, haujawahi kurekodiwa katika historia.

 

Tags