Maziko ya mashahidi wa Muqawama yafikisha vilivyo ujumbe kwa walimwengu
(last modified Tue, 25 Feb 2025 06:14:50 GMT )
Feb 25, 2025 06:14 UTC
  • Maziko ya mashahidi wa Muqawama yafikisha vilivyo ujumbe kwa walimwengu

Wakati utawala wa Kizayuni na mabeberu wa dunia wanapowaua kigaidi viongozi wa Muqawama, huwa wanajidanganya kwamba wamepata ushindi. Hii ni kwa sababu maadui hao hawajua falsafa ya kuuawa shahidi katika njia ya Haki.

Mamilioni ya watu waliojitokeza kwenye maziko ya mashahidi wakubwa wa Muqawama wa Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Safiyyuddin ni ushahidi mwingine wa kuonesha kuwa ndio kwanza mti mtakatifu wa Muqawama unaanza kuatika maua. Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za shughuli hiyo ya mazishi iliyovunja rekodi za kila upande: