Maelfu ya Wazayuni waandamana tena dhidi ya Netanyahu
(last modified Sun, 03 Nov 2024 11:43:57 GMT )
Nov 03, 2024 11:43 UTC
  • Maelfu ya Wazayuni waandamana tena dhidi ya Netanyahu

Maelfu ya walowezi wa Kizayuni wameandamana dhidi ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walikusanyika mbele ya makao makuu ya Wizara ya Vita ya Israel na kupiga nara dhidi ya Netanyahu.

Walowezi hao wa Kizayuni wameandamana wakilalamikia sera na siasa za Benjamin Netanyahu na kutoa mwito wa kufikiwa makubaliano ya ubadilishanaji mateka na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Maandamano hayo yanajiri sambamba na kushadidi malalamiko ya familia za mateka wa Kizayuni wanaoshikiliwa na harakati yay HAMAS.

Malalamiko ya familia za mateka wa Kizayuni dhidi ya Netanyahu ni mwendelezo wa kushadidi hasira na hitilafu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kwa kuahidi kuwatimua Hamas kutoka Gaza, alipanua wigo wa vita katika ukanda huo katika hali ambayo leo hii makundi ya muqawama ya Palestina, Lebanon na eneo yamewapa Wazayuni mapigo makali yasiyoweza kufidika.

Licha ya indhari na maonyo ya baadhi ya viongozi wa Kizayuni, lakini Wazayuni wenye kufurutu ada wanaunga mkono kuendelea vita huko Gaza katika hali ambayo mamlaka za kiusalama na kijeshi za utawala wa Kizayuni zinatahadharisha vikali kuhusu madhara makubwa ya vita hivyo.