HAMAS: Andamaneni na zidini kuzizingira balozi za utawala wa Kizayuni na wanaouunga mkono
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa wito wa kuzidishwa harakati za umma katika ngazi ya kimataifa katika kulaani mwendelezo wa jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuliunga mkono taifa la Muqawama la Palestina.
Katika wito wake huo, Hamas imewataka walimwengu walaani zaidi kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, kuzingirwa kikamilifu eneo la kaskazini la ukanda huo, na kukazania utawala huo ghasibu kuendeleza vita vya mauaji ya kimbari na kuwatesa kwa njaa raia Wapalestina wasio na ulinzi katika eneo hilo; na vilevile kuanika hadharani na kulaani uungaji mkono wa Marekani, Uingereza na Ujerumani kwa wavamizi wa Kizayuni katika vita na uchokozi wao dhidi ya Ghaza.