Matokeo muhimu ya uchunguzi: Kizazi Z kinachukia bidhaa za Israel
Uchunguzi uliofanywa kkatika maeneo mbalimbali na matokeo ya kura ya maoni vinaonyesha kuwa bidhaa zinazotengenezwa na Israel zina hadhi ya chini sana kati ya watumiaji wa kimataifa.
Tovuti ya Kizayuni ya Globus imekiri kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel uko katika nafasi ya mwisho katika kategoria ya chapa ya ndani.
Uchunguzi uliofanywa katika miezi ya hivi karibuni kati ya watu 40,000 katika nchi 20 kuhusu viashiria sita vya nguvu ya chapa, kama vile siasa, utamaduni, watu, mauzo ya nje, uhamiaji na utalii, umefichua kuporomoka huko kwa hadhi ya bidhaa za Israel.
Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti ya Al-Mayadeen, matokeo ya tafiti hizo yanaonyesha kuwa kizazi kipya (Gen Z) kinaupinga vikali utawala wa Kizayuni wa Israel na kinaupa utawala huo alama ya chini zaidi katika maeneo yote.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa vikwazo dhidi ya bidhaa za Israel vimeweka mauzo ya Tel Aviv katika hatari kubwa. Imesema bidhaa ambazo zina alama ya kutengenezwa katika maeneo yanayokaliwa kwa mapavu na Israel zinachukiwa sana na Gen Z.
Wakati huo huo, Moti Sharaf, mwanzilishi wa Kampuni ya Israel Brands, ambayo inafanya kazi ya kukuza chapa hizo duniani, amekiri kwamba alama za biashara za Israel zimekuwa katika hali mbaya sana tangu kuanza kwa vita huko Gaza.
Siku chache zilizopita Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali huko Gaza ilisema kuwa vita vya maangamizi vilivyoanzishwa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza vimeua shahidi zaidi ya Wapalestina 61,000, na kuwalazimisha wengine zaidi ya milioni mbili kuwa wakimbizi. Gaza
Wapalestina wengine 14,222 bado wako chini ya vifusi vya majengo au barabarani, na maiti zao bado haziijakusanywa.
Idara hiyo imesema kuwa jeshi la Israel limeua na kufuta kabisa familia 2,092, na limeua familia nyingine 4,889 ambazo zimeacha mtu mmoja tu kwenye kila familia katika uhalifu uliotajwa kuwa ni maangamizi ya kizazi.