Sababu gani zimepelekea kuongezeka biashara ya nje ya Iran?
Takwimu zinaonyesha kuwa, biashara ya nje ya Iran imefikia dola bilioni 104.
Ripoti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Biashara ya Iran inaonyesha kuwa, katika kipindi cha miezi kumi iliyopita, majimui ya biashara ya nje ya nchi ilikuwa tani milioni 158 na 180,000 yenye thamani ya dola bilioni 103 na milioni 846.
Kulingana na ripoti hiyo, mauzo ya nje ya nchi yasiyo ya mafuta yamefikia takribani dola bilioni 48 katika miezi kumi iliyopita, ambayo ni ongezeko la 18% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Ushirikiano na majirani daima umekuwa ndio kipaumbele cha siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka ya hivi karibun. Katika muktadha huo, harakati za kutafuta njia za kupanua ushirikiano wa pande mbili zimekuwa ndio lengo kuu la viongozi wa Iran na nchi jirani.
Kuzingatia uwezo mkubwa wa kiuchumi wa eneo hili na ukaribu wa jiografia na kuweko mshabaha na mfanano wa kiutamaduni, wa kilugha na kiutamaduni kumeiweka Iran na majirani zake kwenye njia ya kupanua ushirikiano.
Anuawai kwa anuwai ya soko katika maeneo ya kaskazini, kusini, mashariki na magharibi mwa Iran ni fursa mwafaka kwa makampuni ya viwanda ya Iran kukidhi mahitaji yao kwa kuendelea kushauriana na kuzingatia mahitaji ya majirani zao kwa kuzalisha bidhaa bora pamoja na kuwa na uwepo mkubwa katika masoko lengwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran, kati ya jumla ya biashara ya nje ya nchi, zaidi ya tani 127,396,000 zenye thamani ya dola 47,755,000,000 zilitengwa kwa mauzo ya nje katika kipindi cha miezi 10 ya mwaka huu, ambayo iliongezeka kwa 12% katika suala la uzito na 18% katika suala la thamani.
China ikiwa na dola bilioni 12.3, Iraq dola bilioni 10, Umoja wa Falme za Kiarabu ikiwa na takriban dola bilioni 6 na Uturuki dola bilioni 5.5 ndizo sehemu kuu za mauzo ya nje ya Iran ya bidhaa zisizo za mafuta.
Bidhaa kuu zinazouzwa nje ya Iran ni bidhaa za petrokemikali. Katika kipindi hiki, tani 30,783,000 za bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 56 ziliingia Iran, ambayo inaonyesha kupungua kwa 3% katika suala la uzito na ongezeko la 3% kwa upande wa thamani.
Katika kipindi hiki, bidhaa kuu zilizoagizwa na Iran kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, Uchina, Uturuki na Ujerumani zilikuwa dola.
Kwa kuongezeka kwa maingiliano ya kisiasa kati ya Iran na Saudi Arabia, uhusiano wa kibiashara pia umeongezeka. Takwimu zinaonyesha kuwa, mauzo ya Iran ya tani 58,971 kwa Saudi Arabia yalikuwa na thamani ya dola 23,319,448, ikiwa ni ongezeko la 99% ikilinganishwa na mwaka jana.
Mbali na mauzo ya mafuta na gesi na bidhaa za petrokemikali ambazo ni sehemu kuu ya mauzo ya Iran, katika miaka ya hivi karibuni makampuni na taasisi zingine za kiuchumi hapa nchini pia zimeanzisha mpango mpana wa kuingia katika masoko mapya. Kuongezeka kwa mabadilishano ya kibiashara ya Iran na nchi jirani na bara la Afrika kumepelekea kukua kwa kiasi kikubwa mauzo ya bidhaa za Iran na hivyo kuliongezea taifa hili pato la fedha za kigeni.
Makampuni na taasisi kubwa za umma na za binafsi za Iran zimezingatia anuwai na utofauti katika uzalishaji wa bidhaa kama stratijia yao kuu ya shughuli za kiuchumi, na njia hii imekuwa na taathira chanya katika kutambulisha uwezo wa kiuchumi na usafirishaji wa nchi hii.
Uwepo amilifu na hai wa makampuni ya Kiirani katika maonyesho ya kieneo na kimataifa (maonyesho makubwa yanayoangazia uchumi na teknolojia) kumepelekea kutambulishwa bidhaa za ubora wa juu za Iran na kuyafanya makampuni makubwa na yanayotambulika kimataifa kuvutiwa na bidhaa za taifa hili.
Uchumi wa Iran, tofauti na miaka ya nyuma, hautegemei bidhaa moja tu, kwani hii leo kuna aina mbalimbali za bidhaa zinazozalishwa na kutengenezwa na makampuni na taasisi za kiuchumi za nchi hii.
Kujikita wauzaji bidhaa wa Iran katika masoko ya kieneo pia kumeongeza mauzo ya bidhaa nje, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu na ya kimsingi katika kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya nchi jirani. Makampuni ya Iran pia yamewekeza katika miradi mikubwa ya miundombinu nje ya mipaka ya nchi.
Kwa kuzingatia uwezo wa ndani wa malengo ya kiuchumi ya Iran hilo nalo litapelekea hali hii kuchukua mkondo wa kukua. Hii ni katika hali ambayo, Marekani na nchi za Magharibi zinaendelea na vitendo vyao vya uhasama na uadui dhidi ya Iran.
Ukuaji mkubwa wa biashara ya nje ya Iran, licha ya vikwazo hivyo, ni ithbati tosha ya kutokuwa na taathira mwenendo huo wa adawa na chuki. Weledi wa mambo wanaamini kwamba, Iran imeweza kugeuza vikwazo hivyo na kuwa fursa. Nafasi na umuhimu wa kistratijia na kimkakati wa Iran umekuwa sababu ya kupanuka ushirikiano wa kiuchumi na nchi za eneo na sehemu mbalimbali za dunia.