Mwezi wa Ramadhani Gaza: Wapalestina wataabika kuandaa futari na daku
Vita haribifu vya utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Ukanda wa Gaza vimekuwa na taathira nyingi kwa wakazi wa eneo hilo katika siku za nyuma hususan katika kiipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ripoti kutoka Gaza zinaeleza simulizi chungu ya wakazi wa Gaza katika mwezi wa Ramadhani kutokana na kuendelea kuhama makazi yao, ukosefu wa chakula na ukosefu wa maji na umeme.
Ripoti hizo zinaeleza kuwa, wakazi wa Gaza wanakipitisha kipindii hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye magofu ya nyumba na katika mahema yaliyochakaa katika vituo vya makazi, wakitumai kuwa mwezi wa Ramadhani utakuwa dawa ya maumivu na huzuni ya kupoteza wapendwa wao na nyumba zao.
Wakazi wa Ukanda wa Gaza wana hali mbaya kutokana na ukosefu wa maji na umeme na ukosefu wa chakula, na misururu mirefu hupangwa mbele ya maduka ya mikate na matanki za maji.
Wengi hupata shida sana kupata maji wakati wa mfungo huu wa Ramadhani na hulazimika kusubiri kwa masaa kadhaa mbele ya vituo vya misaada kupata chakula.
Familia nyingi za Waislamu katika Ukanda wa Gaza zinashindwa kujikimu futari na daku wakati huu wa Ramadhani huku bidhaa za chakula nazo zikiadimika na kushuhudiwa mfumuko mkubwa wa bei.
Wakati wa adhana ya magharibi inapoadhiniwa na wenye Saumu kuwa na ruhusa ya kufuungua Swauumu zao kwa mujibu wa mafundiisho ya Kiislamu, baadhii ya familia hukaa na kutazamana tu wakisubiri huenda atatokea mtu awapatie chochote ili waweze kufuturu.Wakati wa daku pia hali ni hivyo hivyo.