Mkuu wa Umoja wa Maulamaa aghadhibishwa vikali na kimya cha Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na Ghaza
Apr 20, 2025 02:24 UTC
-
Sheikh Ali Qaradaghi
Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu amekosoa vikali kimya cha Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Waislamu Wapalestina wa Ghaza.
Sheikh Ali Qaradaghi, Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu, ametoa taarifa yenye maneno makali akiutaka umma wa Kiislamu na dhamiri ya utu na ubinadamu zichukue hatua za haraka sana kuhusiana na maafa ya kibinadamu yanayoendelea kujiri huko Ghaza.
Katika taarifa yake hiyo, Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu amesema: "Enyi Umma wa Kiislamu! Ewe dhamiri iliyo hai ya ubinadamu! Hadi lini mtaendelea kuwa kimya?! Ni nini tena kimebaki cha kukupeni msukumo ili mkomeshe uchokozi huu wa kinyama?! Ghaza iliyojeruhiwa imeteketezwa na kuharibiwa kikamilifu mbele ya macho ya ulimwengu. Karibu watu laki mbili wameuawa shahidi na kujeruhiwa, huku njaa na maradhi yakichukua roho za mayatima na wenye misiba".
Sheikh Qaradaghi amesisitiza kwa kusema: Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu na mahala pa Mi'raji ya Mtume (SAW), unanajisiwa na uvunjiwa heshima kila siku asubuhi na jioni, bila kujali dini wala dhamiri ya utu.
Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu amewahutubu Waislamu kwa huzuni na ghadhabu akisema: "Hadi lini? Ni nani? Ni nani? Mko wapi? Liko wapi jibu la utoaji msaada kwa kilio cha wanaoomba kusaidiwa?!.../