Mkutano wa Kiislamu Lahore watilia mkazo kuungwa mkono Palestina
Mkutano wa Kiislamu kuhusu nafasi ya ulimwengu wa Kiislamu katika kuunga mkono Palestina uuliofanyika huko Lahore, Pakistan umetilia mkazo juu ya uulimwengu wa Kiislamu kuunga mkono kadhia ya Palestina.
Mkutano huo ulioshirikisha shakhsia wa ndani na wa kieneo umefanyika Lahore, Pakistan, ili kuchunguza nafasi ya ulimwengu wa Kiislamu katika suala la Palestina.
Shakhsia wenye vipaji wa kisiasa na kidini walioshiriki katika mkutano huo walichunguza nafasi ya ulimwengu wa Kiislamu katika suala la Palestina katika mazingira ya sasa.
Asghar Masoudi, Balozi Mdogo wa Iran mjini Lahore, alimwambia ripota wa Al-Alam: "Ulimwengu wa Kiislamu lazima udumishe umoja wake dhidi ya tishio la Wazayuni - ambalo linazidi kuongezeka kwa uungaji mkono wa Marekani - na leo hakuna nafasi ya kukwepa." Aliongeza: "Gaza inatoa wito kwa kila mtu."
Samer Adnan Hamadah, mwakilishi wa Taasisi ya Marafiki wa Palestina pia amesema: "Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu unaweza kufanya mengi kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni, jambo dogo zaidi kati ya hayo ni kufikisha misaada ya kibinadamu na kutumia mashinikizo ya kisiasa na kimataifa kwa utawala huo ili ufungue kivuko cha Gaza, kwa sababu hali ya eneo hilo ni mbaya sana na wananchi wanahitaji kila kitu ikiwemo maji, chakula na dawa."
Kwa mujibu wa ripoti, washiriki wa mkutano huo wamelaani jinai za utawala wa Kizayuni na Marekani huko Palestina, Lebanon na Yemen na vitisho vyao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza ulazima wa kukabiliana na utawala huo ghasibu.