Mashambulizi dhidi ya Meli ya Uhuru; Jinai nyingine ya Israel
(last modified Sun, 04 May 2025 09:43:53 GMT )
May 04, 2025 09:43 UTC
  • Mashambulizi dhidi ya Meli ya Uhuru; Jinai nyingine ya Israel

Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya jinai nyingine ya kushambulia kwa droni na ndege zisizo na rubani meli za uhuru (Freedom Flotilla) iliyokuwa inapeleka misaada ya kibinadamu kwa wananchi madhlumu wa Ghaza, na hivyo kuzidisha orodha ya jinai za utawala huo katili dhidi ya ubinadamu.

Meli iliyokuwa inaelekea Ghaza Palestina kwa ajili ya kuwafikishia misaada ya kibinadamu wananchi wa ukanda huo ilivamiwa na kushambuliwa na droni yaani ndege ziziso na rubani za Israel kwa ghafla moja na kwa makusudi. Mbali na jinai hiyo kuhatarisha maisha ya watu 30 waliokuwemo kwenye meli hiyo, lakini pia imeonesha namna ukatili wa Israel usivyo na kikomo na jinsi utawala wa Kizayuni usivyojali roho ya mtu yeyote yule. Kuzamishwa na Israel meli iliyokuwa inapeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, kunaonyesha kuwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza mbali na kwamba hazina kikomo lakini pia kiburi hicho kisingeshuhudiwa kama si msaada wa pande zote wa Marekani kwa utawala huo katili mtenda jiinai.

Wanawake na watoto wadogo, wahanga wakuu wa jinai iza Israel ambayo inawatesa watu hawa madhlumu kwa kiu na njaa na unashambulia na kuzamisha hata meli zinazowapelekea misaada

 

Meli hiyo iliyokuwa na misaada ya kibinadamu imezamishwa na utawala wa Kizayuni katika hali ambayo, kwa mujibu wa taasisi za kimataifa, hiyo ni moja ya jinai mbaya sana kuwahi kufanywa dhidi ya ubinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limeonya kuhusu kuendelea kuzingirwa kila upande Ukanda wa Ghaza likisema: "Hakuna msaada wowote ulioingia Ghaza kwa karibu miezi miwili, na kwamba njaa, kiu na maradhi vinaendelea kuwatesa wakazi wa ukanda huo." UNRWA imeongeza kuwa, akiba ya chakula walichokuwa wanasambaziwa wananchi wa Ghaza inaelekea kumalizika kabisa. Malori ya misaada iko kwenye mpaka wa Ghaza kusubiri kuruhusiwa kuingia kwenye ukanda huo lakini Israel hairuhusu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA na mashirika mengine ya kibinadamu yana misaada mingi ya kuokoa maisha ya wananchi wa Ghaza na tayari imeshafikishwa kwenye mipaka ya ukanda huo. Vivuko vya mpakani lazima vifunguliwe tena. Watu wa Ghaza hawawezi kusubiri zaidi ya hapa. Watu wa Ghaza wanafanyiwa jinai za kivita kila sekunde. Miripuko ya mabomu inasikika kila siku na wakazi wa ukanda huo hawafikishiwi msaada wowote.

Meli ya Misaada ya Kibinadamu iliyoshambuliwa na Israel Ukanda wa Ghaza

 

Suala jengine muhimu la kuligusia hapa ni kwamba, kuzamishwa na Israel meli hiyo ya msaada hasa katika hali ambayo madhumuni yake yalikuwa ni kupeleka misaada kwa watu wanaohitajia mno msaada huo, kunaonesha wazi jinsi utawala wa Kizayuni ulivyo na kiburi cha kupuuza sheria za kimataifa na haki za binadamu. Hatua hiyo ni jinai nyingine ya kivita inayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza. Kwa upande wake, Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa na kusisitiza kwa kusema: "Shambulio dhidi ya meli ya kiraia iliyobeba misaada ya kibinadamu ni ukiukaji wa wazi wa sheria, desturi na maadili ya binadamu ya kimataifa, na inathibitisha kwa mara nyingine kwamba utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina ni utawala wa kifashisti usioheshimu maazimio yoyote ya kimataifa, hautambui chochote isipokuwa ugaidi na ukaidi, na una kiu isiyokatika ya kumwaga damu za watu wasio na hatia na kufanya uharibifu."

Nukta nyingine muhimu kuhusu jinai hiyo ya Israel, ni kwamba jinai hiyo na pia kuendelezwa mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza na kuwatesa kwa makusudi kwa njaa na kiu wakazi wa ukanda huu, kunadhihirisha udhaifu wa jamii ya kimataifa mbele ya ukiukaji wa haki za binadamu na jinai za kivita za Israel. Kushindwa jamii ya kimataifa kukomesha ukaidi na jinai za utawala wa Kizayuni, kivitendo kumepelekea kudharauliwa jamii hiyo katika pembe zote za dunia. Aidha ni lazima kusema hapa kwamba shambulio la meli ya "Freedom Flotilla" si tu ni uhalifu dhidi ya ubinadamu bali pia ni jinai ambayo inapaswa kuamsha hisia za kibinadamu za jamii ya kimataifa. Jamii ambayo katika miongo ya hivi karibu iimekuwa ikidai kuwa inafanya kazi ili kukuza utu wa binadamu duniani. Aidha inabidi walimwengu wazidi kuamka na kuelewa kwamba uungaji mkono wa madola ya Magharibi hususan Marekani kwa jinai za utawala wa Kizayuni ndiyo sababu kuu ya kuendelea jinai za Israel ambazo kivitendo zinakejeli madai yanayotolewa na jamii hiyo ya kuhimiza kuheshimiwa ubinadamu kimataifa.