Afisa wa Kizayuni: Israel inaua watoto wachanga kwa ajili ya burudani
-
Yair Golan
Mkuu wa Chama cha Democrats cha Israel amekosoa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni na kusema: "Israel inaua watoto wachanga kwa ajili ya kujifurahisha, na mwenendo huu unaonyesha kutengwa na kukataliwa kwa utawala huo kimataifa."
Yair Golan, mkuu wa Chama cha Democratic, alitoa kauli tata jana Jumanne akikosoa sera za baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu akisema: "Kama Israel ingekuwa na busara, isingeua watoto wachanga kwa ajili ya burudani." Golan aliongeza kuwa: "Israel inasonga mbele katika njia ambayo itasababisha kukataliwa na kutengwa kimataifa, kama ilivyokuwa Afrika Kusini katika miaka iliyopita."
Meja Jenerali Yair Golan amelikosoa baraza la mawaziri la Israel akisema: "Baraza hili limejaa watu wanaopenda kulipiza kisasi na wasiozingatia maadili."

Golan ameonya kuwa Israel inaelekea kutengwa na kuanguka katika ngazi ya kiuchumi na kijamii, na kupoteza uwezo wake wa kudhamini usalama kwa Waisraeli, na kwamba Israel itakuwa mahali pagumu pa kuishi.
Afisa huyo wa Israel ameendelea kumkosoa Netanyahu kwa kukubali matakwa ya mawaziri wa fedha na usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni na kusema: "Netanyahu ni mchezaji mdogo aliyefeli katika zama za Trump."